Arsenal itakuwa dimbani bila ya kiungo Mathieu Flamini katika mchezo wao wa hivi punde dhidi ya Borussia Dortmund imethibitika.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 29 alipatwa na maumivu katika mchezo dhidi ya Norwich ambao Arsenal walishinda kwa mabao 4-1 na sasa analazimika kupumzishwa.
Winga Theo Walcott naye atakosekana kutokana na matatizo madogo ya tumbo na atasalia nje ya uwanja.
Arsenal v Dortmund head-to-head
Katika michezo minne ya huko nyuma waliyokutana Arsenal imeshinda mara mbili na Dortmund wakishinda mara moja na mchezo mmoja wakienda sare.Hawa wote watakosekana
Yaya Sanogo (back), Lukas Podolski (hamstring), Alex Oxlade-Chamberlain and Abou Diaby (both knee) watakuwa nje.
Wenger anasema
"Flamini anaendelea vizuri. Amefanya mazoezi lakini hatacheza".
Arsenal ndio vinara wa ligi ya England na wanaongoza kundi la ligi ya mabingwa baada ya ushindi mara mbili katika michezo ya ufunguzi.
Dortmund wako nyuma kwa alama tatu baada ya ushindi mara moja na kichapo mara moja.
No comments:
Post a Comment