Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limefanya mabadiliko kwa kiingilio cha
juu cha mechi ya raundi ya mwisho ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza
Fainali za Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 kati ya
Tanzania (Serengeti Boys) na Congo Brazzaville itakayochezwa Jumapili
(Novemba 18 mwaka huu).
Awali
kiingilio cha juu katika mechi hiyo itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni kilikuwa sh. 5,000. Lakini kwa
lengo la kuwafanya wadau wa kiingilio hicho kuchangia gharama za mechi
hiyo sasa kutakuwa na viingilio vitatu tofauti katika viti vya VIP.
Kwa
VIP A ambayo ina viti 748 kiingilio kitakuwa sh. 10,000, VIP B
inayochukua watazamaji 4,160 kiingilio ni sh. 5,000 wakati VIP C yenye
viti 4,060 kiingilio ni sh. 2,000. Kwa sehemu nyingine (viti vya rangi
ya chungwa, kijani na bluu) ambavyo jumla yake ni 48,590 kiingilio
kitabaki kuwa sh. 1,000.
Timu
ya Congo Brazzaville kwa taarifa tulizopata awali kutoka Shirikisho la
Mpira wa Miguu la Congo (FCF) ilikuwa iwasili jana (Novemba 13 mwaka
huu) usiku. Lakini timu hiyo haikutokea na sasa tunatarajia itawasili
leo (Novemba 14 mwaka huu) saa 8 mchana kwa ndege ya Ethiopian Airlines.
Congo itafikia Sapphire Court Hotel.
No comments:
Post a Comment