KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, November 27, 2012

KIM POULSEN: NITAWAGONGA TU BURUNDI SINA SHAKA YOYOTE.



Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Bara ( The Kilimanjaro Stars) Kim Poulsen amesema amesha isoma vizuri timu ya taifa ya Burundi na sasa anasubiri kuwafunga.

Pambano hilo litapigwa hapo kesho kwenye dimba la Uwanja wa Namboole ukiwa ni mchezo wa pili baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Sudani Kusini mchezo uliopigwa jumapili iliyopita.

Pambano hilo linatarajiwa kuwa ugumu wa aina yake kwakuwa linazikutanisha timu ambazo zote zilianza kwa matokeo ya ushindi ambapo wao Burundi walianza kwa kuwaning'iniza Somalia kwa mabao 5-1.

Timu yoyote itakayo shinda katika mchezo huo itakuwa imefuzu moja kwa moja kucheza hatua ya robo fainali kwani itakuwa imefikisha alama sita.

Kim Poulsen alitumia muda wa takribani dakika 45  kuzishuhudia Burundi na Somalia na baada ya hapo alisikika akisema kazi imekwisha.
 "Nimeziangalia timu hizi ambazo tuko katika kundi moja kwa dakika 45 nadhani kazi imekwisha, Burundi wana mchezo mzuri lakini wana makosa mengi ya kimchezo hivyo nitatumia makosa yao kupata ushindi"
"Ninakikosi kizuri ukilinganisha na jinsi walivyocheza hawa na ninakiamini"

"Kikosi changu kina wachezaji vijana ambao kila siku wanabadilika na wanajiamini sina shaka hata kidogo na uwezo wao na nina matumaini tutawashinda na kusonga mbele katika hatua ya robo fainali,".

Kim pia alisifu ushirikiano wa winga Mrisho Ngasa na mshambuliaji John Bocco akisema utazaa matunda mazuri katika kikosi chake.
"Ngasa na Bocco wanafanya kazi nzuri naamini wakiendelea na ushirikiano huu mambo yatakuwa mazuri zaidi kwetu,".alisema Kim.

No comments:

Post a Comment