Kamati maalum iliyoundwa na rais wa shirikisho la soka
nchini Tanzania TFF Leodigar Tenga ambayo iko chini ya mwenyekiti Ridhiwani Kikwete kwa
ajili ya kuhakikisha Timu ya Taifa ya vijana ya Serengeti Boys inashinda, imesema imefanikiwa kukusanya shilingi
milioni 35 kati ya shilingi milioni 162 zinazo hitajika katika kampeni ya
kufanikisha Serengeti boys inafuzu fainali za mataifa ya Afrika kwa vijana.
Akiongea na waandishi wa habari hii leo makamu mwenyekiti wa
kamati hiyo Kassim Dewji amesema fedha hizo kimsingi zimetokana na michango ya
wanakamati wenyewe huku kamati yake ikikutana mara tatu tangu kuteuliwa kwake kuangalia
masuala muhimu katika kuhakikisha timu ya vijana ya Serengeti inapata ushindi kwa michezo yote miwili dhidi
ya vijana wenzao kutoka Congo Brazzaville.
Amesema kimsingi wameigawa bajeti katika sehemu kuu mbili
ambapo katika mchezo wa kwanza bajeti yake ni shilingi milioni 60 na sehemu
iliyosalia itaingia katika bajeti ya maandalizi ya mchezo wa pili.
Kassim ameitaja mikakati ya kamati yake kuwa ni pamoja na
kutoa motisha kwa vijana hao kuhakikisha wanapata ushindi na kwamba watanzania
wanamategemeo makubwa kutoka kwao.
Aidha amesema katika siku tatu za mwisho
kabla ya mchezo kambi ya timu hiyo itahamia katika hoteli ya JB Belmont.
Pia amesema mkakati mwingine ni kuangalia uwezekano wa
kuboresha huduma nyingine ndogondogo ili kuwapa nguvu wachezaji.
Pamoja na hilo pia wamewaandalia chakula cha jioni siku ya
ijumaa ili kuzungumza nao na kuonyesha ni namna gani wanavyo wasapoti.
Kamati hiyo pia imepanga kufanya mapokezi mazuri kwa wageni
wao timu ya Congo Brazzaville ambao wameshawasili tangu jana na wamefikia
katika hoteli ya Saphire sambamba na mapokezi mazuri kwa waamuzi ambao
watawasili kesho kutoka nchini Uganda.
Dewji amewataka watanzania kufahamu umuhimu wa mchezo huo
ambao ni wa kihistoria kwani endapo vijana hao watapata matokeo mazuri dhidi
ya Congo baada ya michezo yote miwili ya
nyumbani na ugeinini , itakuwa imefuzu kwa mara ya kwanza katika fainali hizo
ambazo zinatarajiwa kufanyika mwakani nchini Morroco ambapo nchi nne za juu
baada ya michuano hiyo zitakuwa zimefuzu kucheza kombe la dunia la vijana.
Amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi uwanjani siku ya
mchezo kwa lengo la kuwashangilia vijana wao jambo ambalo litawapa nguvu uwanjani.
Dewji alifuatana na wajumbe wengine wa kamati hiyo akiwemo
Salim Said,Abdalah Bin Kleb, Angetile Oseah na Henri Tandau.
No comments:
Post a Comment