KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, December 24, 2012

AISHA MADINDA AFANIKIWA KUACHA NA KUTOA SUMU YA MADAWA YA KULEVYA MWILINI KWAKE SASA AANZA KAZI YA KUTOA DARASA, AMPONGEZA RAY C KWA KUFANIKIWA KUACHA.

  BAADA ya kutumia dawa za kuondoa sumu ya madawa ya kulevya mwilini mwake, aliyekuwa Mnenguaji wa Bendi ya African Stars "Twanga Pepeta", Mwanaisha Mohammed Mbegu ‘Madinda’ (Aisha Madinda) amegeuka kuwa muhamasishaji kwa ‘mateja’ ambao bado wanatumia ‘unga’.

Akizungumza na mtandao wa Bendi ya Afrikan Stars "Twanga Pepeta", Aisha amesema ingawa bado anaendelea kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kumeza dawa za kumaliza kabisa sumu ya madawa hayo pia ameanza kazi ya uhamasishaji wa kuacha kutumia madawa hayo katika Shirika la Kudhibiti Madawa ya Kulevya na Ukimwi (PHRP) lililopo Kinondoni.

Aidha, alisema kazi hiyo ya uhamasishaji anaifanya kwa wiki mara tatu ambapo ni Jumatatu, Jumatano na Ijumaa. Alisema  hutoa somo kwa waathirika wa unga wanaoishi katika kituo hicho.
 
 Amesema kuwa somo analotoa linahusu umuhimu wa kuzingatia dawa na jinsi ya kusahau utumiaji wa unga kwa vile imebainika kuna wakati waathirika walioamua kuacha, hutamani kuendelea kutumia.

“Namshukuru Mungu sasa hivi kipimo cha dawa kimepungua kwa sababu nilipoanza nilikuwa nakunywa kikombe kizima, kwa sasa nakunywa nusu kutokana na afya yangu kuendelea vizuri, lakini pia nimekuwa muhamasishaji wa PHRP kwa kutoa somo kwa waathirika,” alisema.

Alimpongeza mwanamuziki wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ kwa uamuzi wake wa kukubali kuanza kutumia dozi ambapo sasa afya yake imerudi vizuri

No comments:

Post a Comment