Mlinda mlango
nambari moja wa Real Madrid skipper Iker Casillas amekataa kukosoa maamuzi ya
kocha wake Jose Mourinho kufuatia kocha huyo mreno kuamua kumuweka benchi
katika mchezo ambao Madrid ilipigwa bao 3-2 na Malaga mchezo wa mfululizo wa
michezo ya ligi kuu ya nchini Hispania La Liga.
Maamuzi ya
kumuweka benchi Casillas alielezewa na kocha huyo kuwa ni maamuzi ya kiufundi
lakini kichapo toka kwa Malaga kiliishtua klabu hiyo katika dimba la La
Rosaleda.
Kocha anaamua
nani wa kucheza. Ninapaswa kufanya mazoezi sana katika hali kama hii ya
kiushindani na Adan.
"Mourinho
hakuniambia lolote na hajaelezea lolote.
Hakuwahi kunipa maelezo ya lita
litacheza, kwa hiyo sijui lini nitacheza.
"wachezaji
wenzangu wote wananipa sapoti kama ilivyo kwa Antonio [Adan]. Matokeo yetu
hayakuwa mazuri, lakini ukweli ni kwamba sisi wote tunapata sapoti kwakuwa wote
ni wamoja."
Taarifa za
kuwekwa benchi kwake hazikuwa ni za kushtusha kwani alikwisha kufahamu tangu
katikati ya wiki kuwa huenda akawekwa benchi.
Casillas anaanimi
ushindani uliopo baina yao unapswa kuimarika zaidi ili aweze kufanya jitihada
kurejea katika milingoti mitatu.
No comments:
Post a Comment