KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, December 27, 2012

FRANSIC CHEKA AFANIKIWA KUCHEKA NDANI YA BOXING DAY BAADA YA KUMTWANGA CHOTKA CHIMWEMWE WA MALAWI NA KUTWAA MKANDA WA IBF AFRIKA UWANJA WA SHEIKH AMRI ABEID KALUTA MKOANI ARUSHA.

Meya wa jiji la Arusha Gaudence Lyimo na rais wa TPBC Onesmo Ngowi wakimvisha mkanda Francis Cheka mkanda wa ubingwa wa IBF baada ya kumtwanga mpinzani wake Chotka Chimwemwe wa Malawi kwa points katika pambano lililochezwa katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Kaluta mkoani Arusha.
Fransic Cheka akitupa konde zito kwa Chimwemwe ambaye naye anaonekana akikwepa.
Frincis Cheka akikwepa konde zito la Chimwemwe.
Msemaji wa shirikisho la soka nchini Bonface Wambura alikuwa ni mmoja wa majaji wa pambano hilo hapa akitafakari kitu kabla mpambano kuanza.
Hapa ni muda mfupi kabla ya kutangazwa mshindi.
Makonde yakirushwa na mabondia Chotka Chimwemwe mwenye bukta ya mchirizi mwekundu(kulia) na Fransis Cheka bukta ya mchirizi mweupe (kushoto) akilitazama konde hilo kwa makini.
Meya Gaudence Lyimo akimvisha mkanda Cheka.
Bondia Francis Cheka amefanikiwa kushinda pambano lake la kuwania ubingwa wa IBF Afrika baada ya kumpiga kwa pointi bondia toka Malawi Chiotka Chimwemwe kwenye pambano la raundi 12 lililofanyika kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.

Majaji wa pambano hilo ambao walikuwa watatu walitoa alama kama ifuatavyo: David Chikwanje alimpa Cheka pointi 112/114 za Chimwemwe, Boniface Wambura alimpa Cheka pointi  118/114 za Chimwemwe na James Ligongo alimpa Cheka pointi  120/115 za Chimwemwe

Cheka ambaye alipigwa konde la haja likasababishwa kuchanika katikati ya paji la uso katika raundi ya pili aliweza kurejea mchezoni na kuhimili maumivu na hatimaye kumaliza raundi zote huku akitibiwa kila baada ya round moja.

Baada ya Mpambano kumalizika Cheka allisema anashukuru ameshinda ila mpambano ulikuwa mgumu sana kwake na alikiri hajakutana na bondia mkali kama Chimwemwe kwa karibuni.

 "Nashukuru nimeshinda ila nimeshinda kwa bahati kwani bondia niliyekutana naye ni bondia mzuri kwani angeweza kushinda ila alikosa mbinu chache tu", alisema Cheka.

Naye bondia Chiotka Chimwemwe alikubali matokeo na kusema ni mara yake ya kwanza kupigana nje ya nchi yake  hivyo amechukulia kama changamoto kwake.

Cheka ameweza kutwaa Ubingwa wa IBF Afrika baada ya kunyang'anywa kwa kushindwa kuutetea kwa muda na akaenda kucheza na Karama Nyilawila ubingwa wa UBO ambao pia alimpiga Nyilawila.

Naye Meya wa jijini la Arusha  Gaudence Lyimo alimpongeza promota wa pambano hilo Andrew George na Rais wa TPBC Onesmo Ngowi kwa kuleta pambano hilo la kimataifa Arusha na kusema atashirikiana nao kuwahakikisha anainua mchezo wa ngumi Arusha.

"Nawapongeza walioleta pambano hili Arusha nawaahidi tutakuwa tukishirikiana bega kwa bega kuahakikisha tunainua mchezo wa ngumi Arusha", alisema Meya Gaudence.

No comments:

Post a Comment