Winga wa Tottenham
Gareth Bale amefurahia kufanikiwa kufunga mabao matatu ya kwanza katika mchezo
mmoja ‘Hat trick’ katika ligi kuu ya soka ya England ‘Premier League’ lakini
anasema kikubwa ulikuwa ni ushindi ambao uliipatia alama tatu muhimu Spurs
baada ya kuichapa Aston Villa mabao 4-0 hapo jana.
Jermain
Defoe alifunga goli la kwanza kwa Spurs kunako dakika ya 58 kabla ya Bale
kufunga magoli mengine matatu yaliyowapa uhakika wa ushindi katika mchezo huo.
Vijana hao
wanaotoka London ya Kaskazini waliingia katika mchezo huo wakiwa na kumbukumbu
ya sare ya bila kufungana dhidi ya Stoke, ambapo walikuwa wakijua wazi kwamba
muhimu kwao ulikuwa ni ushindi ili kuendelea kuleta ushindani katika nafasi ya
juu katika msimamo wa ligi.
Akinukuliwa kupitia
ukurasa wa mtandao wa kijamii wa twitter wa klabu yake, Bale amesema,
"vizuri kufunga magoli na kupata ‘hat
trick’ yangu ya kwanza katika ‘Premier League’ lakini muhimu ni kupata alama 3".
"wachezaji
wote walifanya kazi nzuri, sasa tunajipanga kwa ajili ya mchezo na Sunderland"
Kwa upande
wake meneja Andre Villas-Boas amepongeza vijana wake walivyokuwa uwanjani tangu
kuanza kwa mchezo mpaka mwisho
Newcastle huenda ikakumbana na rungu
la FIFA.
Newcastle na
Millwall huenda wakakumbana na adhabu ya shirikisho la soka duniani FIFA kufuatia
vilabu hivyo kugomea kuwaachia wachezaji wa kimataifa wa Nigeria Shola Ameobi na Danny Shittu kwa ajili ya
kulitumikia taifa lao katika michuano ya fainali za mataifa ya Afrika nchini
Afrika Kusini mwezi Januari
Bosi wa Newcastle
Alan Pardew anasema mshambuliaji wake Shola Ameobi hatasafiri kuelekea Afrika
katika fainali hizo.
Ameobi na Shittu
wote wanatarajiwa kujitoa rasmi katika uteuzi wao katika timu ya taifa ya
Nigeria (Super Eagles), jambo ambalo limeonekana kulikasirisha shirikisho la
soka la nchi hiyo (NFF).
Meneja wa Newcastle
Alan Pardew amesema Ameobi hatatokezea katika michuano hiyo ambayo inatarajiwa
kuanza January 19, wakati ambapo mlinzi wa Millwall er Shittu naye anatarajiwa
kutolea nje uteuzi wake kama ilivyo kwa Ameobi.
Sheria za FIFA
zinasema mchezaji yoyote ambaye atashindwa kuripoti katika timu yake ya taifa
baada ya kutajwa na nchi yake kwa ajili ya majukumu ya kimataifa , basi
mchezaji huyo atakuwa si halali kutumika katika kipindi chote kilichopendekezwa
wakati wa jukumu hilo pamoja na kuongezewa siku tano zaidi kama itawezekana vinginevyo
kuwepo na makubaliano mengine kati ya klabu yake na nchi husika.
Mjumbe wa
bodi ya shirikisho la soka la Nigeria Chris Green amesema watahakikisha klabu
za wachezaji hao zinaadhibiwa kama watagomea kuwaachia wachezaji hao.
Blackburn yamfuta kazi meneja wake Henning Berg baada ya
kutumikia siku 57 kama bosi.
Blackburn
Rovers imemfukuza kazi meneja wake Henning Berg na maafisa wengine watatu
katika safu ya makocha ikiwa ni hatua ambayo imefuatia klabu hiyo kutereza
katika vibaya katika msimamo wa ligi ndogo ya nchini England, Championship.
Meneja huyo
raia wa Norway, ambaye aliajiriwa mwezi October, katika jumla ya michezo 10
amefanikiwa kushinda mchezo mmoja tu katika kipindi chake cha utumishi wake wa
siku 57.
Berg, ambaye
alikuwa mchezaji wa Rovers mwaka 1995 wakati huo Rovers ilishinda taji la ligi
kuu ya England “Premier League” na
baadaye akishinda taji la “League Cup” akiwa nahodha wa kikosi mwaka 2002, alirejeshwa
katika klabu hiyo kama meneja mwezi Oktoba.
Baada ya Blackburn
kuanza kwa kusuasua chini ya meneja wake wa zamani Lyn Oslo na Lillestrom klabu
hiyo ikaamua kumpa Berg jukumu la kukinoa kikosi hicho katika kipindi hiki cha
mwisho wa mwaka.
Kichapo cha
bao 1-0 kutoka kwa Middlesbrough jana Boxing Day kilipelekea Rovers kujikuta
katika nafasi ya 17 ikifanikiwa kukusanya alama 7 ndani ya uwezo wake wa
kukusanya alama 30 kama wangeshinda michezo yote chini ya meneja Henning Berg.
Meneja msaidizi,
Eric Black, kocha wa namba moja Iain Brunskill kocha wa makipa Bobby Mimms nap
wamekumbwa na dhahma hiyo ya kufukuzwa kazi pamoja na Berg kutoka katika viunga
vya Ewood Park.
Rodgers: hatukustahili lolote dhidi ya stoke city.
Meneja wa Liverpool
Brendan Rodgers amesisitiza kuwa hawakuwa na la kujivunia katika mchezo ambao
walipoteza kwa kuchapwa mabao 3-1 na Stoke City iliyocheza vema hapo jana kule
katika dimba la Britannia jioni ya jana.
Wekundu hao
walipata bao la mapema kupitia kwa nahodha Steven Gerrard kwa njia ya penati
baada ya Luis Suarez kuangushwa katika eneo la hatari na Ryan Shawcross.
Hata hivyo
Stoke wakafanikiwa kusawazisha na baadaye kuandika bao la pili la uongozi
kupitia kwa Jonathan Walters na kisha bao la kichwa la Kenwyne Jones.
Brendan Rodgers
amekiri kikosi chake kuvurunda katika mchezo huo lakini pia akionekana kuhuzunishwa
na aina ya magoli yaliyokuwa yakifungwa na kusema timu yake inapaswa kujifunza
namna ya kulinda kama inataka kupata alama katika michezo ya ugenini.
“ulikuwa ni
mwanzo mzuri kwetu kwa kupata goli la mapema kupitia njia ya penati, lakini tulishindwa
kujilinda nadhani magoli yote matatu na makosa ya ulinzi, kiukweli
hatukustahili chochote katika mchezo huu”
No comments:
Post a Comment