KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, December 23, 2012

PICHA MBALIMBALI ZA MCHEZO WA STARS NA CHIPOLOPOLO. ENJOY.

 Mshambuliaji wa Taifa Stars, Mrisho Ngassa akijiandaa kuachia shuti kali lililoipatia  Stars bao la kuongoza wakati wa mchezo wa kirafiki uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Taifa Stars imeshinda bao 1-0.
 Kipa wa Timu ya Chipolopolo ya Zambia akiruka bila mafanikio kufuata shuti kali lililokiwa limepichwa na mchezaji wa Taifa Stars Mrisho Ngasa.
Mpira ukiwa tayari nyavuni.
 Mshambuliaji wa Taifa Stars,Hamis Mcha (katikati) akiwachachafya mabeki wa timu ya Zambia katika mchezo wa kirafiki uliochezwa jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Taifa stars imeshinda bao 1-0.
 Hamis Mcha (7) akiendelea kuwapa kazi mabeki wa timu ya Zambia.
 Mchezaji wa timu ya Zambia,Moses Phiri (9) akiingia kwenye lango la timu ya Taifa Stas,huku beki wa Stars,Aggrey Moris akijiandaa kukabiliana nae.
 Mchezaji wa timu ya Zambia,Moses Phiri (9) akijaribu kutaka kumtoka beki wa Taifa stars,Salum Aboubakar wakati wa Mchezo wa Kirafiki uliochezwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar.Taifa stars imeshinda kwa bao moja lililotiwa kimiani na Mshambuliaji machachari,Mrisho Ngassa mnamo dakika ya 45 ya mchezo. 
 Ilikuwa ni piga nikupige.
 Mashabiki walijitokeza kwa wingi.
 Waandishi kutoka nchini Zambia wakifuatilia kwa makini mchezo huo.
Hapa suala la ulinzi limewekwa pembeni na kuanza kufuatilia mechi.
 Kocha wa Taifa Stars,Kim Poulsen akipeana mkoni na Kocha wa Zambia ambaye alionekana kutofurahishwa na Matokeo ya kufungwa kwa Timu yake, mara baada ya kumalizika kwa mechi ya Kirafiki iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar jioni hii. Taifa Stars imeshinda bao 1-0.
Kocha wa Zambia hataki kumsikiliza mtu.
King Kim Poulsen akiongea na waandishi wa habari baada ya mchezo.
Waandishi wa habari wakumuuliza maswali King Kim Poulsen baada ya mchezo.
Wachezaji wa Zambia wakiondoka uwanjani kwa aibu kubwa baada ya kuchapwa bao 1-0.
Rais wa chama cha soka cha Zambia Kalusha Bwalya akiongea na waandishi wa habari baada ya mchezo.

No comments:

Post a Comment