KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, December 22, 2012

UKURASA WA HABARI ZA MICHEZO ZA KIMATAIFA: Rodgers: Liverpool itasajili wachezaji wenye njaa tu, Asern Wenger aanza mipasho na wakosoaji wake, Ricaldo Kaka haondoki Madrid nasema Mourinho, Chelsea kumchukua Theo Walcott kuziba pengo la Sturridge na Michael Laundrup anasema Michu ni sawa na Van Persie.



Meneja wa Liverpool Brendan Rodgers ameonya kuwa usajili ndani ya klabu hiyo hautatazama thamani ya mchezaji kwa kigezo cha mshahara na ada ya uhamisho, wakati huu ambapo Liverpool inataka kujirekebisha kutoka katika kipindi kirefu kisichokuwa na mafanikio ambapo ilisajili wachezaji kwa mapesa mengi lakini hakuna walichofanya.


Mpaka sasa wekundu hao bado wanaendelea kuwategemea wachezaji waliosajiliwa na meneja aliyetangulia Kenny Dalglish ambao ni Jordan Henderson, Andy Carroll na Stewart Downing ambao kwa pamoja waliigharimu klabu hiyo kiasi cha euro milioni 92.

Ikiwa tayari imesha kamilisha mkataba mwingine wa muda mrefu na Raheem Sterling baada ya mazungumzo ya muda mrefu, Rodgers anasisitiza kuwa anawataka zaidi wachezaji wenye njaa ya mafanikio kuliko wenye zawadi kubwa ya pesa..



Amekaririwa akisema,

"unapaswa kupata wachezaji wenye njaa ambao wanataka kufanya kazi na kupigania mafanikio hilo ndilo kubwa kwangu."

"Hao watapata mikataba mizuri wakija hapa, lakini kama watakuwa wanaulizia pesa na mambo mengine mengi , siwataki, kwa uzoefu wangu wachezaji wa aina hiyo watakuangusha siku tu kwa namna moja ama nyingine.


Kauli hiyo ya Rogers inaarifiwa kuwa imetokana na mazungumzo marefu juu ya Raheem Sterling na uongozi wa klabu hiyo ambapo Sterling alikomaa katika mazunguzo hayo akitaka mshahara wa wiki wa euro elfu 36,800.


Mara baada ya pande hizo kukubaliana na kuingia mkataba wa muda mrefu hapo jana mchana, Sterling aliuambia mtandao wa Liverpool kuwa amefurahishwa na kufikia makubaliano.



Nimeibadilisha Arsenal - Aserna Wenger awajibu wakosoaji wake
 Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa haridhishwi na mwenendo wa Arsenal yake lakini hatakuwa tayari kukubali ukosoaji ambao umekuwa ukielekezwa kwake.


Meneja huyo Mfaransa alijikuta katika wakati mgumua katika miezi ya hivi karibuni kufuatia washika mitutu hao kufungwa na katika mchezo wa robo fainali na Bradford City mchezo wa michuano ya Capital One.


Lakini Wenger ameendelea kujitetea kuwa amekuwa na kazi nyepesi sasa kuliko ilivyokuwa huku nyuma wakati akianza.

Akiongea na The Mirror amesema,

“Siridhishwi na hali ya mambo, najitahidi kufanya kila niwezalo na naamini nitafanikiwa na hata nikiondoka niwe nimefanya."

“nimekuwa katika ukosoaji mkubwa katika kipindi cha miaka saba iliyopita , lakini kama meneja ilikuwa ni ngumu zaidi mwaka wa kwanza nilipoanza hapa,

“ninachoami pia ni kwamba klabu imekuwa tangu nilipowasili. Ukilinganisha na tulipo sasa na tulipotoka unaweza kuona hiyo tofauti.

 “Nilipowasili klabu ilikuwa Highbury ambapo kulikuwa hakuna viwanja vya mazoezi na ilikuwa na waajiriwa 80 .

“Leo kuna waajiriwa karibu 500 na tunachezea uwanja mkubwa  na kituo kikubwa cha mazoezi.

“Na pia klabu klabu inayojulikana dunia nzima. Tumekuwa katika vilabu vinavyo cheza kwa kiwango cha juu”


Arsenal inakaribia kufikisha miaka minane bila ya taji lakini Wenger anasisitiza kuwa anajivunia uasisi wake wa uwanja mkubwa wa Emirates ambao anadhani ni jambo kubwa kuliko makombe.



 Mourinho anasema Kaka haondoki Bernabeu. 
 Kocha wa Real Madrid Jose Mourinho amesema haamini kama Rocaldo Kaka ataondoka Santiago Bernabeu katika kipindi cha uhamisho kinachokuja licha ya tetesi kusikika.


Mshambuliaji  huyo mwenye umri wa miaka 30 alikuwa akihusishwa na kutana kuelekea Corinthians na New York Red Bulls, lakini kocha wa Madrid anataka mshambuliaji huyo wa zamani wa AC Milan kusalia katika mji mkuu wa Hispania Madrid.


Amenukuliwa Mourinho katika mkutano na waandishi wa habari akisema,

"sidhani kama kitafanyika kitu mwezi January, na sidhani kama Kaka ataondoka".

"Endapo atasalia itakuwa jambo zuri kwa timu".

Mourinho pia amezungumzia juu ya maamuzi ya shirikishp la soka Ulaya ‘Uefa’ kuipiga faini na kuwafungia wapinzani wao wa mchezo wa leo katika mchezo wa ligi ya Hispania La Liga Malaga.


Malaga imeondolewa katika michuan o ijayo ya vilabu ya Uefa licha ya kufuzu hii ikiwa ni kutokana na kushindwa kufikia kigezo cha mahitaji ya pesa.


"Ni jambo baya sana unafuzu uwanjani lakini kwasababu ambazo si za kimichezo unaondoshwa mashindanoni, hii inawahuzunisha mashabiki".



Chelsea inamtaka Walcott, Pjanic & Willian kuziba nafasi ya Sturridge.
 Chelsea imewajumuisha Theo Walcott, Willian na Miralem Pjanic katika orodha fupi ya wachezaji walio katika mpango wao kuziba nafasi ya Daniel Sturridge.


Mabigwa hao wa soka Ulaya wanataka mtu wa pembeni ambaye ataruhusu mpango wa mahitaji ya meneja wao Rafael Benitez wa kuwa na washambuliaji wanao zunguka.


Chelsea imeendelea kuwepo kileleni katika mbio za kumsaini Falcao kutoka Atletico Madrid licha ya kwamba huenda huenda asijiunge na timu hiyo mpaka majira mengine ya kiangazi lakini pia wanamtaka mshambuliaji mwenye uwezo wa sehemu yoyote katika eneo la ushambuliaji.


Taarifa za uhakika zinasema klabu hiyo yenye maskani yake katika jiji la London imethibitisha kumjumuisha mshambuliaji wa  Arsenal Theo Walcott, mshambuliaji wa Shakhtar Donetsk, Willian na mwingine ni mshambuliaji wa AS Roma, Pjanic.


Sturridge amekuwa kwenye mpango wa kuondoka Stamford Bridge na kwasasa yuko katika mazungumzo na ya kutaka kuelekea Liverpool mwezi ujao kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni £12.


Walcott anaweza kuelekea jijini London kama atashindwa kuafikiana na mambo mbalimbali na Arsenal, licha ya kwamba Arsene Wenger kukaririwa akisema mshambuliaji huyo wa kimataifa wa England hatauzwa.


Willian, winga wa Brazil ambaye aliisumbua sana Chelsea katika mchezo wa vilabu bingwa Ulaya hatua ya makundi anaendelea kuwepo katika darubini ya mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich licha ya euro milioni €25 kukataliwa na Shakhtar.



 Michael Laudrup Van Persie sawa na Michu
 Michael Laudrup amekipongeza kiwango cha Michu msimu huu kiasi kupelekea kumlinganisha mshambuliaji wa kimataifa wa Hispania na Manchester United Robin van Persie.


Mshambuliaji huyo wa Swansea na mdutch Van Persie wote wamefunga magoli 12 katika ligi kuu ya England msimu huu na wanaungana katika kitabu cha wafungaji bora.


United itakuwa ikielekea katika dimba la Liberty hapo kesho na Laudrup anahofia uwezo wa Van Persie, lakini anaamini kikosi chake kinaweza kuibuka na ushindi endapo wataendelea na utamaduni wa kujiamini na kucheza kwa uwezo wao.


“United ina wachezaji wenye kiwango na wasiofanya makosa katika eneo la hatari kama Van Persie.

“unapaswa kuwa makini naye wakati wote kulinda vizuri na kuwa na hadhari ya kudondosha mipira karibu.

“Michu na Van Persie wako sawa. Ni kama wanafanana wote wanapiga miguu ya kushoto, hawana kasi lakini wanajua niwakati gani wa kukimbia.

No comments:

Post a Comment