KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, December 22, 2012

MWAMUZI KINDA WA MICHUANO YA UHAI MCHEZO WA AZAM NA MTIBWA MICHUANO YA UHAI AOKOLEWA NA MAKOMANDOO WA TFF. FAINALI KESHO AZAM NA COAST UNION.




 
 
  Vurugu kubwa ziliibuka jana katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya michuano ya Uhai baina ya Azam na Mtibwa Sugar, ambapo mwamuzi wa mchezo huo kijana mdogo Listoni Hyalu alinusurika kupata kipondo toka kwa mashabiki waliohudhuria mchezo huo.  

Kisa na mkasa wa kuibuka kwa vurugu hizo ni kutokana na mwamuzi huyo kukataa goli la penati ambalo lingeamua matokeo ya mwisho ya mchezo huo ambapo pengine mtibwa walikuwa mbele kwa penati 2-1 na kwakuwa mchezo ulikuwa katika hatua ya penati ya piga nikupige mwamuzi alipaswa kuashiria mpira kumalizika lakini kwa mastaajabu ya wengi alikataa penati hiyo.

 Mwamuzi aliikataa penati hiyo kwa madai kuwa mlinda mlango alicheza katika mstari wa goli kabla ya mpigaji kupiga, licha ya kwamba mpigaji alifunga penati yake na pengine ingekuwa  advantage au faida kwa mpigaji kwakuwa aliyefanya kosa ni mlinda mlango na hivyo kuashiriaki mpira kumalizika.

Maamuzi ya mwamuzi yakapelekea penati hizo kuendelea kupigwa na hatimaye Azam wakafakiwa kupata penati nyingine ya kusawazisha kabla ya kupiga nyingine ya ushindi, na hivyo kusonga mbele kwa hatua ya fainali.

Ndani ya dakika 90 za mchezo matokeo yalikuwa 1-1

Baada ya filimbi ya kuashiria mchezo umekwisha mashabiki walivamia uwanja kwa lengo la kumuadabisha mwamuzio huyo kinda kwa madai kuwa aliibeba Azam kwa maagizo ya kuwalinda kwa kuwa ndio wadhamini wa michuano hiyo kupitia bidhaa yao ya maji ya Uhai.

Hata hivyo kwa msaada wa makomandoo wa TFF ambao walikuwepo uwanjani mwamuzi huyo akanusurika na kipigo hicho.

Hali ilizidi kuwa mbaya zaidi pale mashabiki hao baada ya kumkosa mwamuzi Listoni Hyalu wakataka kulivamia basi la Azam ambalo lilikuwa likiwachukua wachezaji wa Azam ambao nao waliamua kushuka kutoka kwenye gari hilo na kuanzisha varangati lingine la mawe na michanga, lakini viongozi wa Azam wakafanikiwa kutuliza munkari ya wachezaji wao hali ya mambo kutulia.

Matokeo ya Azam kuifunga Mtibwa kwa mbinde kunapelekea
Azam ya Dar es Salaam na Coastal Union ya Tanga ndizo zitakazoumana kwenye fainali ya michuano ya Kombe la Uhai 2012 itakayochezwa kesho jioni (Desemba 23 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam.

Coast Union waliwafunga Simba kwa mabao 2-1 mchezo uliopigwa uwanja wa Karume jana jioni.

Mechi ya fainali itaanza saa 10 kamili jioni, na itatanguliwa na ile ya kutafuta mshindi wa tatu kati ya Mtibwa Sugar na Simba ambayo itachezwa saa 2 kamili asubuhi kwenye uwanja huo huo.

Mbali ya kombe, bingwa wa michuano hiyo atapata sh. milioni 1.5, makamu bingwa sh. milioni 1 wakati mshindi wa tatu atajinyakulia sh. 500,000. Timu iliyoonesha zaidi mchezo wa kiungwana (fair play) itapata sh. 400,000, mchezaji bora wa mashindano sh. 350,000, mfungaji bora sh. 300,000 na kipa bora sh. 300,000.

Naye kocha bora katika mashindano hayo atazawadiwa sh. 300,000 kama itakavyokuwa kwa refa bora.

No comments:

Post a Comment