
Zambia imekuwa
ni bingwa wa kwanza katika fainali za mataifa ya Afrika kuondolewa katika
mzunguko wa kwanza katika kipindi cha miaka 21 ya michuano hiyo baada ya kwenda
sare ya bila kufungana na Bukina Faso mchezo wa kundi C wa michuano hiyo
inayofanyika nchini Afrika kusini.
Mazingira kama
hayo yaliwahi kuwakuta Algeria, ambao walishindwa kutinga hatua kama hiyo mwaka
1992 wakiwa ni mabingwa watetezi.
Wakati Zambia
wakishindwa kufanya hivyo, wao Nigeria wamefanikiwa kushika nafasi ya pili
katika kundi hilo baada ya kuifunga Ethiopia kwa mabao 2-0 katika mchezo
mwingine uliochezwa katika muda unaofanana kuepusha upangaji wa matokeo mjini Rustenburg.
Matokeo hayo
yameifanya Nigeria na Bukina Faso kulingana kwa alama wote wakiwa na alama tano
lakini wakizidiana kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa.
Bukinabe
sasa wanamsububiri mshindi wa pili wa kundi D ambaye atapatikana hii leo kati
ya Togo au Tunisia.
Katika mchezo
huo Collins Mbesuma aliungana na mshambuliaji wa Southampton Emmanuel Mayuka katika
sehemu ya ushambuliaji ya Zambia, ambapo mshambuliaji huyo wa Orlando Pirates
Mbesuma alikuwa akicheza nafasi ya nahodha Christopher Katongo ambaye unahodha
wake ulikaimiwa kwa muda na mlinda mlango Kennedy Mweene.
Kocha Herve
Renard alifanya badiliko moja la mchezaji pale alipomuingiza Hichani Himonde aliyechukua
nafasi ya mlinzi mkongwe Joseph Musonda.
Kwa upande
wa Bukinabe nahodha Moumouni Dagano aliendelea kusugua benchi kwa mara ya pili
na nafasi yake kuchukuliwana Benjamin Balima.
Mlinda mlango
Daouda Diakite alikuwa katika milingoti mitatu ya goli la Bukina Faso huku
mlinda mlango namba moja Abdoulaye Soulama akiaangalia mpira kama mtazamaji
kufuatia kusimama kwa mchezo mmoja baada ya kusimamishwa kwa kadi nyekundu na Florent
Rouamba kuingizwa uwanjani kuchukua nafasi ya Aristide Bance.
Wakicheza katika
vazi la rangi ya manjano na michirizi ya kijani Zambia walipata nafasi nzuri ya
kuandika bao kunako dakika ya 17 pale ambapo kosa ya mlinzi wa Bukina Faso Mady
Panandetiguiri lilipelekea mpira kunaswa na Mbesuma, lakini shuti lake
lilikwenda moja kwa moja katika mikono ya mlinda mlango wa Mali, Diakite.
NIGERIA YAFUZU BAADA YA KUICHAPA ETHIOPIA.
Penati mbuli
za dakika za mwisho mwisho zilizo pigwa na Victor Moses kunako dakika za 79 na
90 zimeisaidia Nigeria kukata tiketi ya kucheza robo fainali ya michuano ya
mataifa ya Afrika baada ya kuibuka na ushindia mabao 2-0 dhidi ya Ethiopia.
Endapo Nigeria
ingekwenda sare ya bila kufungana katika mchezo huo ilikuwa dhahiri shahiri
wako nje ya michuano hiyo kutokana na sheria ya mfumo wa mchezo wa kiungwana (fair play system), ambapo bingwa
mtetezi Zambia angefaidika na sheria hiyo.
Baada ya
kuona dakika zikiyoyoma huku matumaini ya kupata bado yakitoweka, mashabiki wa Nigeria
walianza kukata tama kufuatia timu yao kupata kazi ya kusawazisha katika dakika
la mwisho michezo miwili iliyotangulia.
Hatimaye
bahati ikawadondokea Nigeria kunako dakika ya 79 kufuatia kuangushwa chini
katika eneo la hatari mshambuliaji Victor Moses na mlinzi Alula Girma kabla ya
Moses mwenye kupiga penati hiyo na kuandika bao la kwanza.
Moses
aliwahakikishia Nigeria alama tatu muhimu baada ya mlinda mlango wa Ethiopia Sisay
kufanya madhambi ya kumkwatua mshambuliaji wa Nigeria katika eneo la hatari
ambapo alitolewa nje kwa kadi ya pili ya njano ambao ilizaa kadi nyekundu na
nafasi yake kuchukuliwa na Hintsa lakini Moses akafanikiwa kuandika bao la pili
na kuifanya Nigeria kufuzu.
No comments:
Post a Comment