Kikosi
cha Young Africans Sports Club kimeendelea na mazoezi yake leo katika
uwanja wa Fame Residece Football uliopo Antalya kisha jioni timu ikaenda
kufanya mazoezi katika ufukwe wa bahari, eneo lililopo nyuma ya hoteli
Fame Residence ikiwa ni siku ya tatu katika ziara ya mafunzo nchini
Uturuki kujiandaa na mzunguko wa pili wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara.
Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga mholanzi Ernie Brandts
amesema anafurahishwa na maendeleo ya kambi, kwani toka wameanza mazoezi
jumatatu leo ni siku ya tatu wakiwa nchini Uturuki na anaona mabadiliko
makubwa kwa wachezaji wake, huku akisema hofu iliyokuwepo kwa
watanzania juu ya hali hewa ya baridi kali si kweli kwani hali ya hewa
katika mjii huu ni baridi kiasi tu na hata leo katika mazoezi ya asubuhi
palikuwa na jua.
Wachezaji wanaendelea kuzoea
mazingira, na kujifunza mambo mengi yanayohusu soka kwani wageni
mbalimbali waliofika katika mji huu wamekuwa wakipenda kujua mengi
kuhusiana na timu ya Young Africans na soka la Tanzania kwa ujumla.
Kocha
wa makipa wa timu ya Bayern Leverkusen Detier Gansi jioni alishuhudia
Young Africans ikifanya mazoezi ya ufukweni ambapo alisema amefurahia
kuifahamu timu ya Yanga na wachezaji wake wanaonekana kuwa na morali ya
kucheza soka, hivyo anaamin ziara hii itaisaidia timu kuwa pamoja na
kujiandaa vyema na ligi leoleo asubuhi uwanja wa Fame Residence Footbal.
Wakati
huo huo mchezaji wa kimataifa wa timu ya Taifa ya Rwanda Haruna
Niyonzima amewasili jioni hii kuungana na wenzake kufuatia kuchelewa
kuunganisha ndege siku ya jumamosi usiku akitokea nchini Rwanda
alipokuwa amekwenda kuchezea timu yake ya Taifa.
No comments:
Post a Comment