Mabingwa wa soka Tanzania bara Simba wameanza veam michuano ya kombe la mapinduzi baada ya kufanikiwa kuifunga Jamhuri ya Pemba kwa mabao 4-2 katika mchezo uliopigwa
katika uwanja wa Amani Zanzibar.
katika mchezo huo ambao ulikuwa ni wa heshima ya uzinduzi wa michuano hii ya mwaka huu 2013 ambayo ni kuelekea katika sherehe za maadhimisho ya miaka 49 ya mapinduzi ya Zanzibar ulianza kwa huku mvua ikinyesha na kufunguliwa na makamu wa kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamadi.
Jamhuri ndio walikuwa wa kwanza kuzifumania nyavu za Simba kwa bao lililofingwa na Mfanyeje Musa kabla ya Simba kusawazisha kupitia kwa Athumani Chanongo.
Jamhuri kupitia tena kwa Mfanyeje Musa wakafanikiwa kuandika bao la pili kabla ya Chanongo kusawazisha na timu hizo kwenda mapunziko zikiwa sare ya bao 2-2.
Kipindi cha pili Simba ilifanikiwa kuandika mabao mawili yaliyofungwa na mzambia Felix Sunzu na nahodha Shomari Kapombe.
Mapema kulikuwa na mchezo kati ya Tusker
na Bandari ambapo Tusker imeishindilia Bandari karamu ya mabao 5-1,
yalifungwa na Jesse Were dakika za 29 na 43, Ismail Dunga 35 Michael
Olunga dakika ya 89 na Andrew
Tolowa dakika ya 90 na bao la kufutia machozi la Bandari lilifungwa na
Amour Janja dakika ya
83.
No comments:
Post a Comment