Kufuatia kugongwa na kibonde, Benitez atete uchaguzi wake wa wachezaji.
Meneja wa Chelsea
Rafael Benitez ametetea mabadiliko yake aliyoyafanya kuelekea kwenye mchezo
dhidi ya QPR mchezo ambao Chelsea ilichapwa kwa bao 1-0 na timu ambayo iko
mkiani katika msimamo wa ligi kuu ya England hapo jana.
Ryan
Bertrand, Marko Marin, Victor Moses, Oscar na Ross Turnbull walikuwa ni
miongoni mwa wachezaji waliongezwa na Benitez katika kikosi chake tofauti na
kile kilicho ibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya 2-1 mwishoni mwa juma.
Bernitez anasisitiza
isingekuwa rahisi kuendelea kutumia wachezaji walewale waliotumika katika kipindi
chote cha sikukuu na kudai kuwa Chelsea inapaswa kucheza mpira hata itawakosa
watu kama Juan Mata na Eden Hazard.
"tulikuwa
tunafanya vizuri na tulikuwa tunajiamini na mambo yalikwenda vizuri, tumebadili
baadhi ya wachezaji lakini katika wachezaji wote hao tuliowabadili ni Marko
Marin peke yake ndiye amekuwa hachezi mara kwa mara, Oscar alikuwa anacheza.
"ungeona
baadhi ya wachezaji walivyokuwa wamechoka, hatukuwa na uwezo wa kumiliki mpira,
hatukuwa tunapasiana mpira kwa uhakika na jazba ilikuwa inatawala, mwishowe
tumefanya makosa na tumewapa nafasi, kulikuwa na mambo mengi hatuku yafanyia
kazi.
"QPR walikuwa
wamejipanga na walikuwa wanasubiria na walikuwa wanacheza mchezo wa kushambulia
kwa ghafla(counter attack) na kutengeneza jambo ambalo limeleta tofauti mwisho
wa mchezo.
"hatuwezi
kutumia wachezaji walewale kila siku katika kila mchezo. Kama tunacheza na timu
ambayo iko mkiani nyumbani unatakiwa kuwaamini wachezaji wako na ndivyo
nilivyofanya"
Wakati Daniel
Sturridge akikamilisha uhamisho wake wa kuelekea Liverpool, Fernando Torres alilazimika
kuanza katika kikosi cha kwanza.
Benitez anaamini
akimpata Demba Ba Chelsea italazimika kumpumzisha Torres.
Siku moja baada ya kumsajili Sturridge, Rodgers amchimba mkwara.
Meneja wa Liverpool Brendan Rodgers amemuonya
mchezaji wake mpya Daniel Sturridge ya kwamba yuko katika nafasi ya mwisho wanapo zungumzia klabu kubwa duniani hivyo anapaswa kukaza msuli.
Sturridge
mwenye umri wa miaka 23, amekuwa ni mchezaji wa kwanza wa kusajiliwa na Rodgers mwezi January
baada ya kukamilisha taratibu zote zilizo gharimu uhamisho wa pauni milioni £12
akitokea Chelsea na akisani kwa mkataba wa muda mrefu.
Lakini baada
ya kupata nafasi ya kuanza katika jumla ya michezo 31 ya ligi katika kipindi cha miaka 3 akiwa
na Chelsea na huku mara zote akipangwa kama winga ya kulia badala kucheza kama
mshambuliaji wa kati, Rodgers anaamini mchezaji huyo wa kimataifa wa England anaweza
kutumia vema fursa aliyoipata ya kucheza vizuri katika viunga vya Anfield.
"tumemchukua
mchezaji ambaye anatakiwa kufanya kazi kama anataka kuwa ndani ya moja ya klabu
kubwa duniani"
Rodgers amesema
"kama atataka kuwa katika kiwango bora,
hii ni nafasi yake ya mwisho. Na hiyo ndiyo moja ya sababu"
QPR inamtaka Ben Haim
Meneja wa Queens
Park Rangers Harry Redknapp amethibtisha kuwa klabu yake imedhamiria kumpa
mkataba Tal Ben Haim mpaka kumalizika kwa msimu.
Tal Ben Haim
ameripotiwa kupokea pauni milioni £36,000 kwa wiki akiwa Portsmouth.
Ben Haim
ambaye ana umri wa miaka 30, kwasasa ni
mchezaji huru baada ya kuihama Portsmouth majira ya kiangazi na amekuwa akifanya
mazoezi na QPR tangu mwanzoni mwa mwezi December.
Amenukuliwa Redknapp
akisema baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Chelsea jana usiku.
"Tal amejituma
sana katika kipindi cha mazoezi na tunaangalia kumpa mkataba mpaka mwisho wa
msimu"
Nyota huyo
wa kimataifa wa Israel alianza kugusa soka la England mwaka 2004 alipojiunga na Bolton,
na baada ya hapo alijiunga na Chelsea, Manchester City, Sunderland na hivi
karibuni akitokea Portsmouth.
Pardew: Demba Ba anaelekea
Chelsea.
Bosi wa Newcastle
United Alan Pardew ana matumaini kuwa atazoea mazingira hata kama Demba Ba ataondoka
ambapo inaarifiwa kuwa mshambuliaji huyo anaelekea kujiunga na Chelsea.
Demba mwenye
umri wa miaka 27, yuko katika mazungumzo
na Chelsea juu ya kukamilisha taratibu za kujiunga Stamford Bridge baada ya makubaliano kufikiwa ya
gharama za uhamisho ya pauni milioni £7 hapo jana.
Hata hivyo amesema atetereki na kuondoka kwa Ba kwa kuwa klabu hiyi ni kubwa na itaendelea kusonga mbele kama ilivyokuwa huko nyuma.
"tutasonga
mbele hii ni klabu kubwa, ki ukweli klabu hii ni kubwa kuliko mchezaji yoyote
yule"
Ba ameifungia
Magpies magoli 29 katika jumla ya michezo 54 ndani ya kipindi cha miezi 18
alichoitumikia klabu hiyo ya kutoka pande za Tyneside.
Juve katika mazungumzo na nyota wa Athletic
Llorente
Fernando
Llorente anaelekea katika mazungumzo ya kutaka kujiunga na Juventus kwa
uhamisho huru ambapo klabu yake ya sasa Athletic Bilbao ikitangaza kuwa
mabingwa hao wa soka nchini italia wako pia katika mazungumzo ya kumsajili
majira ya kiangazi.
Llorente
mwenye umri wa miaka 27,ameweka wazi kuwa katika miezi ya hivi karibuni hakuwa
na mpango wa kukubali mpango wowote na klabu hiyo toka pande za Basque, na
kwamba kwasasa yuko huru kuongea na klabu yoyote itakayofaaa kwakuwa mkataba
wake unakwenda kumalizika miezi sita ijayo.
Taarifa fupi
iliyotolewa na mtandao wa Athletic imesema "Juventus Football Club imekutana na Athletic
Club hii leo kuzungumzia juu ya kumalizika kwa kipindi cha utumishi wa Fernando
Llorente na klabu yetu June 30 2013, hivyo wameanza mazungumzo na mchezaji huyo
ili kuwaongezea nguvu katika kikosi chao"
Wakati Juve
wakikaribia kumnasa mshambuliaji huyo lakini bado kuna vilabu vingine
vinavyomnyemelea kutoka ‘Premier League’ kama vile Arsenal, Tottenham na Liverpool
na huenda vikawa pia ni vilabu mbadala endapo Juve watachemsha.
No comments:
Post a Comment