Timu
ya Young Africans Sports Club yenye makao makuu yake jijini Dar es
salaam nchini Tanzania siku ya jumamosi itashuka dimbani kucheza mchezo
wa kirafiki na timu ya Arminia Bielefeld ya kutoka nchini Ujerumani,
mchezo utakaofanyika katika mji wa Antalya.
Young
Africans ambayo imeweka kambi ya mafunzo jijini Antalya itatumia mchezo
huo kama fursa pekee ya kuweza kujipima uwezo dhidi ya timu hiyo ya
Ujerumani ambayo pia imekuja kambi ya mafunzo kujiandaa na mzunguko wa
ligi daraja la pili nchini Ujerumani.
Kocha
Mkuu wa Young Africans Ernest Brandts amesema kwao ni furaha kwa kupata
nafasi ya kucheza na timu kubwa kama ya Armini Bielefeld ambayo
inawachezaji wa kiwango cha kimataifa hivyo anaamini utakua ni mchezo
safi na kuwavutia.
Unajua
tuna siku sita (5) tangu tufike hapa mjini Antalya Uturuki na
tumeshafanya mazoezi kwa siku nne (4) hivo fursa ya kupata mchezo wa
kirafiki ni nzuri sana kwetu kwani itanipa nafasi ya kuona wachezaji
wangu wameshayashika kwa kiasi gani mafunzo yangu alisema 'Brandts'
Arminia
Bielefeld imeshawasili mjini Antalya kwa ajili ya kambi yake ya
mafunzo na hivyo kwao pia ni fursa nzuri ya kuweza kujipima uwezo na
timu ya Young Africans ambao ni mabingwa mara 23 katika ligi kuu ya
Tanzania.
Leo asubuhi
Young Africans imeendelea na mazoezi katika viwanja wa Fame Residecne
tayari kabisa kujiandaa na mchezo huo utakaochezwa siku ya jumamosi
mjini Antalya.
Kikosi
cha wachezaji 27 waliopo mjini Antalya wote wako katika hali nzuri na
hakuna maheruhi hata mmoja hali itakayompa kocha Brandts kuamua kumtumia
mchezaji yoyote katika mchezo huo.
No comments:
Post a Comment