KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, January 3, 2013

MARIO BALOTELI AKUNJWA NA MENEJA WAKE ROBERTO MANCINI NA KUZUA BALAA KUBWA BAADA BALOTELI KUMFANYIA "TACKLING" MBAYA SCOTT SINCLAIR. Angalia picha za la valangati hilo.........

Meneja wa Manchester City Roberto Mancini na mshambuliaji anayedhaniwa kuwa ni mkorofi Mario Balotelli hii leo asubuhi wameingia katika vurugu kubwa miongoni mwao.
Bosi wa Manchini alimfuata na kumkunja, kumsukuma na na kumghasi mshambuliaji huyo raia wa Italia mbele ya wachezaji wengine wakati wakiwa katika mazoezi katika uwanja wa mazoezi wa Carrington. 

Baadaye mshambuliaji huyu mwenye umri wa miaka 22 alizuiwa na kuondolewa na baadhi ya viongozi mmoja wapo akiwa ni Massimo Battara, ambao walishtushwa na mzozo huo wakati huu ambapo City inajiandaa na mchezo wa mzunguko wa tatu wa michuano ya FA dhidi ya Watford. 

Inaarifiwa ya kwamba Mancini alikasirishwa na Balotelli baada ya kumfanyia tackling mbaya Scott Sinclair, jambo ambalo sasa linaweka hatma ya baadaye ya mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Italia katika mashaka  makubwa.

Baada ya Mancini kuona tukio alimkimbilia Mario na kuanza kumkunja ikiwa ni pamoja na kumsukuma kwa kutaka kumuangusha chini jambo ambalo hata hivyo alishindwa kutokana na nguvu alizokuwa nazo Balotelli.

Baada ya tukio , Balotelli alichukua gari lake aina ya Bentley G na kuondoka katika uwanja huo wa mazoezi.

Tayari wasiwasi umeanza kujitokeza kama Baloteli atauzwa ama la kwa kuwa tukio hilo litakuwa linaelekea kujenga mahusiano mabaya baina yao.
 
 
 
 

No comments:

Post a Comment