Meneja Roberto Mancini Manchester City amekasirishwa na maamuzi ya mwamuzi
Mike Dean kufuatia kumtoa uwanjani kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja(straight red card) mlinzi
wake tegemeo Vincent Kompany kufuatria kumfanyia “tackling” Jack Wilshere wa Arsenal.
Kadi hiyo itamuweka nje ya dimba kwa michezo mitatu jambo ambalo
litaathiri kikosi City katika changamoto ya kuwania taji licha ya kwamba klabu
imedai kuikatia rufaa.
Amenukuliwa akisema
'hii siyo kadi nyekundu kabisa, haiwezekani nimpoteze mchezaji kwa michezo
mitatu bila sababu. Haikuwa faulo mimi nina umri wa miaka 48, lakini niemona
vizuri sana hii ‘tackling ilikuwa ni ya kimchezo'
No comments:
Post a Comment