MOURINHO ALIKUWA OLD TRAFORD KUCHUNGUZA MBINU ZA MZEE FURGERSON
|
Meneja wa Real Madrid Jose Mourinho jana alikuwa ni miongoni mwa
watazamaji walikuwa uwanjani Old Traford wakishuhudia pambano la mahasimu wa
soka nchini England baina ya Manchester United dhidi ya Liverpool wakati huu
linasubiriwa pambano baina ya timu yake na United mwezi ujao.
Mourinho na meneja wa zamani wa Barcelona Pep Guardiola ni miongoni mwa
makocha wakubwa wenye majina barani Ulaya ambao wanatarajiwa kuhudhuria seminar
ya makocha barani ulaya kupitia chama chao cha mameneja wa ligi kuu (League
Managers' Association (LMA).
Hata hivyo wadau wa soka nchini England wameitafsiri hiyo kama ni mbinu
mbadala ya Mourinho kuichunguza United huku yeye na Guardiola wakihusishwa
kuchukua nafasi ya kumrithi Sir Alex Ferguson katika viunga vya Old Trafford wakati
utakapofika kwa mskochi kuyo kujiuzulu.
Pia meneja wa timu ya taifa ya England Roy Hodgson naye alikuwepo jukwaani
akiangalia viwango vya wachezaji wake Michael Carrick, Steven Gerrard, Tom
Cleverley na wengine wakati huu ambapo England inajiandaa na mchezo wa kirafiki
dhidi ya Brazil mwezi ujao.
Mchezo huo ulimazika kwa united kuchomoza na ushindi wa mabao 2-1 mabao ya United yakifungwa na Van Persie na Vidic na bao la Liverpool likifungwa na Danniel Sturridge.
|
|
Pichani juu Jose Mourinyo akifuatilia pambano la watani United na Liverpool. |
|
Roy Hogdson naye alikuwepo akiwakagua wachezaji wake wa timu ya taifa. |
|
Van persie anatupia bao la kwanza. |
|
Danniel Sturrigde naye anafunga bao pekee la Liverpool. |
|
Nimanja Vidic anafunga bao la pili la United. |
No comments:
Post a Comment