Wenger: Fabregas anaweza kurudi Arsenal.
Meneja wa Arsenal
Arsene Wenger amesema upo uwezekano mkubwa wa kiungo wake wa zamani Cesc
Fabregas kurejea Emirates Stadium.
Fabregas
mwenye umri wa miaka 25, aliichezea kwa miaka minane Arsenal kabla ya kurejea
nyumbani Hispania katika klabu iliyomkuza tangu akiwa mtoto ya Barcelona kwa
ada ya uhamisho ya pauni milioni 30 mwaka 2011.
Wenger anaamini
kuwa kiungo huyo wa kimataifa ya Hispania kwasasa ametulia Camp Nou, na timu
yake ikiongoza ligi ya nchi hiyo Liga lakini bado anaamini anaweza kurejea
kusaini tena Arsenal.
"Sidhani
kama hararejea moja kwa moja iko siku moja " amekaririwa na gazeti la Guardian.
"ni mtu
wa Arsenal. Anaipenda Arsenal na anaangalia kila mchezo wa Arsenal. Lakini bila
shaka Barcelona kulikuwa ndiyo nyumbani alikokulia lazima ukubali hilo.
"Huenda
asije mwakani au miaka miwili au mitatu kwasababu ana uhusiano mkubwa na Barcelona.
Lakini baadaye linawezekana."
Wenger kwasasa
amepata faraja kubwa kwa wachezaji wake vijana waingereza Kieran Gibbs, Carl
Jenkinson, Jack Wilshere, Aaron Ramsey na Alex Oxlade-Chamberlain – kusaini mkataba
mpya na klabu hiyo.
Capello kuhudhuria sherehe za FA.
Meneja wa
zamani wa timu ya taifa ya England Fabio Capello atakuwa ni miongoni mwa watu
watakao hudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 150 ya chama cha soka cha England
jumatano jijini London.
Sherehe hizo
ambazo pia zitahudhuriwa na meneja wa sasa wa England na zitafanyika Connaught
Rooms huko Holborn.
Kwasasa Capello
ni meneja wa timu ya taifa ya Russia, na tayari ameuarifu uongozi wa FA ataudhuria
katika sherehe hizo.
Capello aliondoka kuifundisha England kwa mizengwe mwezi February 2012 baada ya kutofautiana na maamuzi
ya kumvua unahodha John Terry kwa mara ya pili na tangu wakati huo hakuwa na
mawasiliano na FA.
Ikiwa ni
sehemu ya sherehe za maadhimisho ya miaka 150 ya FA, pia kumeandaliwa michezo
miwili ya kirafiki kati ya England na Brazil na mchezo mchezo mwingine kati ya Scotland
dhidi ya jamhuri ya Ireland. Michezo mingine dhidi ya Ujerumani na Argentina inatarajiwa
kuchezwa baadaye mwaka huu.
O'Brien asaini new West Ham.
Mlinzi wa West
Ham Joey O'Brien ameongeza mkataba mwingine na klabu hiyo ambao utamuweka
klabuni hapo mpaka 2016.
O'Brien
akiwa chini ya Sam Allardyce katika klabu ya Bolton alipelekwa Upton Park mwaka
2011 na bosi wa washika nyundo.
Klabu hiyo
imetangaza hilo kupitia ukurasa wake wa Twitter kwa maneno yaliyosomeka “West
Ham United inayofuraha kubwa kutangaza kuwa Joey O'Brien amesaini mkataba mpya
utakamuweka klabu mpaka kiangazi 2016.”
O'Brien
mwenye umri wa miaka 26, ameitumikia timu ya taifa ya jamhuri ya Ireland michezo
mitano na ameitumikia klabu yake michezo 16 huu wa ligi kuu ya England ‘Premier
League’ akifunga magoli mawili.
No comments:
Post a Comment