Ronaldinho amerejeshwa baada ya kutakata vilivyo katika klabu yake ya Atletico Mineiro. |
Ronaldinho ametajwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Brazil chenye jumla ya wachezaji 20 kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya England utakao pigwa katika dimba la Wembley.
Mchezo huo maalum utakao pigwa februari 6 utakuwa ni kwa ajili ya kuadhimisha miaka 150 ya chama cha soka cha England ambapo pamoja na Ronaldinho pia amejumuishwa katika kikosi hicho mlinzi wa Chelsea David Luiz.
Mchezo huo utakuwa unamrudisha Ronadilnho ambaye aliwahi kuwa mchezajo bora wa dunia mara mbili, baada ya kukosekana kwa muda mrefu.
Hii ni orodha ya majina yaliyoidhinishwa na kuwasilishwa katika shirikisho la soka la Brazil. |
Si tu Ronaldinho wengine walioitwa na bosi mpya wa timu ya taifa ya Brazil Luiz Felipe Scolari, ni pamoja na mlinda mlando wa QPR Julio Cesar ambaye naye alipotea kwa kwa muda pamoja na nyota wa Chelsea Ramires na Oscar.
Akiwa katika fomu mlinda mlango wa QPR Julio Cesar sasa arejeshwa na Luis Felipe Scolari.
Taarifa za kutangazwa kikosi cha Brazil zimepokelewa kwa furaha na mashabiki wa soka nchini England kwani wanatarajia kuona vionjo vya wachezaji wanaotajwa kuwa ni bora kwa sasa kama mshambuliaji wa Santos Neymar na wengine wa zamani kama mlinzi wa Barcelona Daniel Alves na Adriano.
Scolari,
ambaye aliiongoza Brazil katika fainali ya kombe la dunia mwaka 2002 amemuacha Ricaldo Kaka na kumpa nafasi mshambuliaji Luis Fabiano kwa kuelekea mchezo huo wa mwezi ujao.
Brazil
itautumia mchezo huo kama sehemu ya maandalizi yao kuelekea katika michuano ya Confederations Cup na kombe la dunia 2014 World Cup.
Kwasasa Scolari ana miezi chini ya 18 kujenga kikosi cha ushindi kitakacho chukua taji la sita katika ardhi ya nyumbani Brazil.
Kikosi kamili ..
Julio
Cesar (QPR), Diego Alves (Valencia); Daniel Alves, Adriano (both
Barcelona), David Luiz (Chelsea), Dante (Bayern Munich), Leandro Castan
(Roma), Miranda, Filipe Luis (both Atletico Madrid); Ramires (Chelsea),
Arouca (Santos), Paulinho (Corinthians), Hernanes (Lazio), Oscar
(Chelsea), Ronaldinho (Atletico Mineiro), Lucas Moura (Paris St
Germain); Hulk (Zenit St Petersburg), Neymar (Santos), Fred
(Fluminense), Luis Fabiano (Sao Paulo).
No comments:
Post a Comment