Rais wa AC
Milan Silvio Berlusconi amesema kuwa klabu yake haina mpango wa kumchukua
mshambuliaji wa Manchester City Mario Balotelli wala kiungo wa Real Madrid Ricaldo
Kaka.
Kauli yake
hiyo inazima uvumi ulikuwepo kuwa walikuwa kwenye mpango wa kumchukua Balotelli
ambaye amekuwa katika sintofanhamu ndani ya klabu yake na kwamba walikuwa
tayari kutoa pauni milioni £20 zikiwa ni taarifa za ndani.
Mialn pia
ilikuwa ikihusishwa kuwepo katika mazungumzo na Real Madrid juu ya uwezekano wa
kumrejesha Kaka San Siro, habari ambazo Berlusconi maezikanusha kwa madai ya
kwamba kwa sasa hawana fedha ya kufanya uhamisho wa aina yoyote.
Akiongea na Radio
2 ya nchini Italia, Berlusconi amekaririwa akisema
"Si Balotelli
wala Kaka atakayekuja Milan. Hizi ni dili zisizowezekana katika kipindi hiki."
Sneijder: Najisikia kama niko
nyumbani ndani ya Uturuki.
Wesley
Sneijder ametanabaisha kuwa anajisikia kama yuko nyumbani akiwa nchini Uturuki.
Kiungo huyo
wa kimataifa wa Uholanzi amejiunga na Galatasaray akitokea Inter Milan mapema
wiki hii kwa ada ya euro €7.5 huku akisema amefarijika kuanza kazi katika timu
yake mpya.
Akiongea na
Galatasaray TV Sneijder amesema
"Huu ni
ujumbe kwa ukaribisho wa aina yake kuwahi kutokea hapa Such an amazing welcome
message could only be seen here, mke wangu Yolanthe ameniambia kuwa nimefanya
maamuzi sahihi'.
"Tangu
tulipowasili tunajisikia kama tuko nyumbani na hili ndio jambo la muhimu,
najisikia raha kuwepo hapa"
No comments:
Post a Comment