TAIFA STARS KUIKABILI CAMEROON ‘FIFA DATE’
Tanzania
(Taifa Stars) itacheza na Cameroon katika moja ya mechi za kirafiki za
Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA)- FIFA Date
zitakazofanyika duniani kote Februari 6 mwaka huu.
Mechi
hiyo itafanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 11
kamili jioni. Kikosi cha Cameroon kinachoundwa na wachezaji wengi wa
kulipwa wanaocheza katika nchi mbalimbali duniani kitaanza kuwasili
nchini Februari 3 mwaka huu.
Nchi
kadhaa ziliomba kucheza na Taifa Stars katika tarehe hiyo ya FIFA,
lakini Kocha wa Stars, Kim Poulsen ameamua kucheza mechi hiyo dhidi ya
Cameroon ambayo nahodha wake ni mchezaji nyota wa kimataifa, Samuel Etoo
Fils.
Congo
Brazzaville, Equatorial Guinea, Rwanda na Swaziland nazo zilikuwa
zimeomba kucheza dhidi ya Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro
Premium Lager. Ukiondoa Swaziland iliyotaka mechi hiyo ichezwe Dar es
Salaam, nyingine zilitaka kucheza nyumbani kwao.
Bofya chini kusikiliza
No comments:
Post a Comment