WAKENYA KUCHEZESHA MECHI YA AZAM
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limewateua waamuzi kutoka Kenya
kuchezesha mechi ya kwanza ya raundi ya awali ya Kombe la Shirikisho
kati ya Azam ya Tanzania na Al Nasir Juba ya Sudan Kusini itakayofanyika
jijini Dar es Salaam kati ya Februari 15 na 17 mwaka huu.
Mwamuzi
wa kati atakuwa Davies Omweno na atasaidiziwa na mwamuzi msaidizi namba
moja Peter Keireini, mwamuzi msaidizi namba mbili Gilbert Cheruiyot
wakati mwamuzi wa mezani Anthony Ogwayo.
Kamishna
wa mechi hiyo atakuwa Hassan Mohamed Mohamud kutoka Somalia. Waamuzi wa
mechi ya marudiano itakayochezwa jijini Juba watatoka Rwanda
wakiongozwa na Gervais Munyanziza.
CAF YATEUA WATANZANIA KUCHEZESHA CAMEROON
Waamuzi
wa Tanzania wakiongozwa na Israel Mujuni wameteuliwa kuchezesha pambano
la awali la raundi ya kwanza kuwania Kombe la Shirikisho kati ya UFC
Haut Nkam ya Cameroon na US Bougouni ya Mali.
Kwa
uteuzi huo wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Mujuni na
wenzake Ali Kinduli, Samuel Mpenzu na Waziri Sheha watachezesha mechi
hiyo itakayofanyika kati ya Februari 15 na 17 mwaka huu.
Pierre
Alain Mouguengui kutoka Gabon ndiye atakayekuwa Kamishna wa mechi hiyo.
UFC Haut Nkam na US Bougouni zitarudiana wiki mbili baadaye nchini
Mali.
No comments:
Post a Comment