KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, January 20, 2013

MKUTANO MKUU WA YANGA KATIKA PICHA MAMBO KADHAA YAJADILI NA KUAZIMIWA NA MENGINE KUPITISHWA( SOMA TAARIFA KAMILI BAADA YA KUANGALIA PICHA CHINI kutoka www.youngafrica.co.tz.))

Klabu ya Young Africans Sports Club leo imefanya mkutano mkuu wa mwaka wa wanachama katika Ukumbi wa Bwalo la Polisi eneo la Oysterbay, huku mkutano huo ukiendeshwa kisasa kwa kuonyeshwa moja kwa moja (live) na kituo cha Luninga cha Clouds nchini kote.
Mkutano ulianza majira ya saa 5 kasoro, huku wanachama wakijitokeza kwa wingi katika mkutano huo ambao ulikuwa haujafanyika kwa kipindi kirefu katika Klabu ya Yanga.
Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Yusuf Manji alifugua mkutano kisha makamu mwenyekiti aliongoza sara kwa upande wa wakristo na mzee Ibrahim Akilimali alisoma dua kwa upande wa dini ya Kiisalamu.
Katika mkutano huo wanachama wameridhia kuongezewa muda wajumbe wa Bodi ya Wadhamini, Mama Fatma Karume na Francis Kifukwe huku wanachama wakipitisha majina ya Captain George Mkuchika na Balozi Ameir Mpumbwe kuwa wajumbe wa Bodi ya Wadhamini.
Uongozi unaandaa taratibu nzuri kwa kadi za uanachama na kwa sasa wapo katika maongezi na baadhi ya taasisi za fedha ili waweze kufanya hivyo, pia katiba inabidi iboreshwe na mkutano mkuu wa wanachama uwe kila baada ya miezi sita (6) badala ya miezi mitatu (3) y ahivi sasa.
Ifuatayo ni vipengele ambavyo wanachama wamevipisha katika mkutano wa leo;
Katiba - Uchaguzi mgombea nafasi ya mwenyekiti awe namgombea mwenza ili wapate fursa ya kutekeleza mipango/malengo kwa pamoja, tofauti na sasa ambapo kila mgombea anakuwa na mawazo na malengo yake.
Pia Mwneyekiti na makamu mwenyekiti watakua na fursa ya kuchagua wajumbe wa kamati ya utendaji kulingana na mahitaji ya kipindi hicho.

Ujenzi wa Uwanja - Kamati ya utendaji inaendelea na mchakato wa kutafuta njia ya kuweza kupata pesa ya kujenga uwanja na eneo la mafia

Mkadirio ya uwanja ni bli 32, ambapo uwanja utakua na uwezo wa kubeba watu elfu arobaini (40,000) ukiwa na eneo la kuegeshea magari na huduma zote za muhimu katika viwanja vya michezo.
Makamu mwenyekiti alipata fursa ya kuwaonyesha wanachama ramani na michoro ya uwanja mpya unaontarajiwa kuanza ujenzi wake mwishoni mwa mwezi wa tano mwaka huu, ambapo uwanja unatazamiwa kujengwa kwa kipindi cha miaka miwili na kampuni ya ujenzi ya BCCG iliyojenga uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Aidha katika mkutano huo Mwesigwa Selestine, Lousi Sendeu na Godwin Muganyizi wamefutiwa uanachama baada ya kuwa wamefungua kesi za madai dhidi ya klabu yao ya Young Africans. 
Manji alisema pia kuahitajika maboresho katika baadhi ya mikataba kama ya TBL, Push Mobile, Pecha (kalenda) na vifaa vya Yanga (jezi,kofia,kalamu,skafu,suaruali za mazoezi nk) ili viweze kuisadia klabu kuweza kujiendesha kulingana na kipato kinachopatikana.
Katika kitengo cha fedha kuna madeni ambayo Yanga inadaiwa na uongozi bado unahitaji kuyafuatilia ili kuweza kujua uhalali wa madeni hayo:
(i)Cross Road - U$1600 (gharama ya ndege kutoka Zambia)
(ii)Holiday Dreamer - U$ 5079 (gharama za ndege kwenda Cairo) 
(iii)Mwesigwa Selestine - milioni 183.4
(iv)Louis Sendeu - milioni 79 
Pia kuna fedha ambazo zimetumika bila ya idhini ya kamati ya utendaji millioni 288 hazina maelezo, milioni 85.6 bila ya idhini ya kamati ya utendaji na milioni 8.6 hazina ushaidi wa matumizi. 
Mwisho Uongozi uliweza kutoa vyeti vya utambuzi kwa baadhi ya wanachama na wachezaji/viongozi kwa mchango wao katika Klabu ya Yanga, waliopewa vyeti hivyo ni:
1.Abdallah Bin Kleb - kongozi anayejitolea sana katika kuhakikisha timu inafanya vizuri na kushinda michezo inayoikabili
2.Shadrack Nsajigwa - mchezaji aliyechezea Yanga kwa muda mrefu (barua na fedha taslimu tsh 1,000,000/=) 
3.Mahmoud Momar Mpogolo - (mtunza vifaa) mfanyakazi wa siku nyingi katika benchi la ufundi (barua na fedha taslimu tsh 1,000,000/=)
4.Stephen Samuel - mwanachama bora na mwenye uchungu na timu ya Yanga (barua na zawadi ya pikipiki mpya)
5.Hayati Isamail Rashid - mwanachama aliyesaidia kupatikana kwa muafaka (barua)
Mwisho mwenyekiti alifunga mkutano kwa kuwashukuru wanachama wote waliojitokeza katika mkutano huo wa leo, ambapo wanachama waliouhudhuria mkutano ni 1440 huku mkutano ukiendeshwa kwa masaa matatu tu (live) moja kwa moja na kituo cha runinga cha Clouds Tv ambayo kupitia kampuni yake ya Prime Time Promotions ndio walikuwa waandaji wa mkutano huo. 

No comments:

Post a Comment