Shujaa wa Bukina Faso mlinda mlango Diakite. |
Timu ya taifa ya Bukina faso imefanikiwa kutinga fainali ya mataifa ya Afrika na sasa wanajipanga kucheza na Nigeria baada ya kuiondosha timu ngumu ya Ghana kwa mikwaju ya penati 3-2 kufuatia kwenda sare ya bao 1-1 ndani ya 120 za mchezo huo wa nusu fainali ya pili.
Ghana ilifanikiwa kupata bao la uongozi kunako dakika ya 13 kufuatia Madi Panandetiguiri kudaiwa kumuangusha Christian Atsu katika eneo la kisanduku cha hatari wakati walipokuwa katika harakati za kuwania mpira ndani ya eneo hilo ambapo mwamuzi wa mchezo aliizawadia Ghana penati.
Penati hiyo ilifungwa na Wakaso
akipiga mpira wa chini kulia mwa mlinda mlango wa Bukina Faso.
Lilikuwa ni goli la 4 kwa Wakaso lakini pia likiwa ni goli lake la 3 akifunga kwa njia ya penati.
Asamoah Gyan pengine angefanya matokeo kuwa 2-0 kunako dakika ya 58 kufuatia kushindwa kumalizia krosi ya Atsu ambapo mpira wake aliopiga ulitoka nje kulia mwa goli la Bukina Faso.
Bao la kusawazisha la Bukuna Faso lilipatikana kufuatia mpira wa pasi wa Agyemang-Badu kumkukuta Aristide Bance ambaye alitumia mwanya uliokuwa mbele yake baina ya walinzi wawili wa kati wa Ghana na kuukwamisha mpira wavuni.
Katika mapigo ya penati Isaac Vorsah aliaanza kuitoa mkosi Ghana kwa kupiga pembeni penati yake.
Penati nyingine iliyo waweka Ghana katika mazingira magumu ilikuwa ni ile ya Emmanuel Clottey wakati Bukina Faso wakikwamisha wavuni penati zao kupitia kwa Bakary Kone, Henri Traore na Bance. Ghana walipoteza penati ya mwisho iliyowapata ushindi Bukina Faso ambayo ilipigwa na Emmanuel Agyemang-Badu na kudakwa na mlinda mlango Dakite.
Bukina Faso sasa watakutana na 'Super Eagles' Nigeria katika mchezo wa fainali Jumapili katika uwanja wa Soccer City ulioko katika kitongoji cha Soweto.
No comments:
Post a Comment