Mfadhili mpya wa Simba Bi. Rahma Alharouz amewataka mashabiki wa klabu hiyo kujitokeza kuishangilia na kuipa nguvu timu yao katika mchezo wao dhidi ya timu bingwa kutoka nchini Angola ya Libolo mchezo ambao utafanyika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam Jumapili.
Huo ni mchezo wa kwanza wa vilabu bingwa barani Afrika ambapo Simba watakuwa wenyeji kabla ya mchezo wa marudiano utakao fanyika nchini Angola wiki mbili zijazo.
Bi Rahma amesema mchezo huo ni muhimu kwa Simba kwani watakuwa wakicheza wakiwa katika uwanja wa nyumbani hivyo watakuwa wakihitaji matokeo mazuri kabla ya mchezo wa marudiano.
Rahma ambaye aliifandhili Simba ilipofanya ziara ya maandalizi kabla ya kuanza mzunguko wa pili wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara, amesema ameitembelea kambi ya timu ya Simba ilipokuwa Arusha na vijana wote wameonyesha kuwa katika ari ya kufanya vizuri, hivyo basi wanahitaji kupata sapoti ya mashabiki wake Jumapili uwanja wa taifa.
Amesema mchezo wa soka siku hizi ni wa jinsia zote na kwamba wanawake kwa wanaume wajitokezea kwenda kuipa nguvu timu yao ili iweze kupata matokea mazuri bila kujali mapenzi ya vilabu kwa kuwa Simba ni mwakilishi wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment