David Haye atangaza kucheza pambano jijini Manchester June 29. |
Bingwa wa zamani wa uzito wa juu wa WBA David Haye amesema amechoka kusubiri pambano dhidi ya mmoja kati ya ndugu wawili wa Klitschko.
Haye mwenye umri wa miaka 32, ametangaza urejeo wake katika ngumi kwenye mkutano wake na waandishi wa habari jijini London bila ya kutaja atacheza na nani katika pambano ambalo litachezwa katika ukumbi wa Manchester Arena June 29.
Pia anatarajia kucheza pambano lingine baadaye mwishoni mwa mwaka huu dhidi ya mmoja kati ya ndugu hao wawili Vitali au Wladimir Klitschko kuwania moja ya mataji makubwa wanayoshikilia.
Amenukuliwa Haye akisema,
'Badala ya kukaa na kusubiri mwaka mwingine mmoja, nataka kurejea tena'
'Ninayo furaha kurejea tena mwaka ni mrefu kusubiri'
Kampuni binafsi ya Haye 'HAYEMAKER' itasaidia kutangaza urejeo wake na kulitangaza pambano hilo la mwezi Juni huku mwalimu wake Adam Booth akithibitisha kuwa wanafanya mazunguzo ya kumsaka mpinzani wake.

Kwa mara ya mwisho Haye kuoanda ulingoni ilikuwa ni mwezi Juni mwaka jana pale alipo mtwanga mwingereza mwenzake Derck Chisora pambano ambalo lilichezwa Upton
Park.
Haye akimchapa Dereck Chisora kwa KO ya raundi ya tano Upton Park
No comments:
Post a Comment