Mchezaji Marysiana Edga akijaribu kumtoka Shani Ally wa Benjamini. |
Wachezaji waliovaa nyekundu ni timu ya Benjamini na njano ni Kinyerezi kabla ya mchezo ambao Benjamini walishind. |
Mchezaji Nusrat Msuya wa Kinyerezi akiwa na mpira wakati wa mchezo wao dhidi ya Benjamini kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari Jangwani Wasichana. |
Mgeni rasmi akisalimiana na wachezaji kabla ya mchezo kuanza. |
MASHINDANO ya Umoja wa Michezo Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA)
wilaya ya Ilala yameanza leo kwa michezo ya soka, netbali, kikapu, wavu
na riadha kufanyika kwenye viwanja vya sekondari za Azania, Jangwani na
Zanaki.
Kwenye viwanja vya Azania walianza kwa kufukuza upepo ambapo wasichana na wanavulana walikimbia kwenye mbio za mita 100, 200 na 800 na washindi kupatikana.
Baadae ulifika wasaa wa soka ambapo timu za Beenjamin walicheza na Kinyerezi na mpaka Lenzi ya Michezo inatoka uwanjani hapo Kinyerezi ilikuwa inaongoza kwa bao 1-0 huku Cluster ya Upanga na Ilala wao wakiwa bado hawajafungana.
Kwa upande wa netbal Benjamini iliifunga Kinyerezi.
Awali akifungua mashindano hayo Mwenyekiti wa Umuja wa Wakuu wa shule za Sekondari za Ilala aliwataka wachezaji kuwa na nidhamu kwenye michezo kwani kama utashindwa darasani michezo inaweza kukuajiri.

No comments:
Post a Comment