Kiungo wa mashetani wekundu Manchester
United Ryan Giggs anaamini anaamini kabisa kuwa inawezekana kwasasa mchezaji
kuwa na nguvu ya kucheza soka mpaka katika umri wa miaka ya mwishoni ya
thelathini kutegemeana na aina ya mikataba na maendelao ya kiteknolojia.
Giggs aliyeanza kucheza soka katika
klabu ya Machester United mwezi mwaka Machi 1991 akiwa na umri wa miaka 17 na
sasa ni zaidi ya miaka 22, bado anaonekana ni mwenye nguvu na msimu huu
amekamilisha jumla ya michezo elfu moja.
Nyota huyo wa zamani wa kimataifa wa Wales,
tarehe mosi mwezi huu amesaini tena mkataba wa mwaka mmoja na United mkataba ambao
utamfanya kuwa ni mchezaji wa tatu kufikia umri wa miaka 40 akiwa kama
ilivyokuwa kwa akina Teddy Sheringham na Gordon Strachan, jambo ambalo anaamini
ni la kawaida.
Wakati United ikielekea katika
michezo miwili migumu dhidi ya Sunderland jumamosi na baadaye katika uwanja wa Stamford
Bridge kukabiliana dhidi ya Chelsea mchezo wa robo fainali ya michuano ya FA, Giggs
analiangalia jambo hilo la kucheza michezo yote miwli ndani ya kipindi cha siku
tatu kwake litakuwa ngumu.
Wilshere huenda akasubiri sana kufuatia maumiu ya kifundo cha mguu.
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amesema
kuwa majeraha yanayomkabili kiungo wake kiungo wake mahiri Jack Wilshere huenda
yakamuweka nje ya uwanja kwa muda mrefu.
Wilshere mwenye umri wa miaka 21
aliondolewa katika kikosi cha timu ya taifa ya England kuelekea katika michezo
miwili ya kuwania kufuzu fainali ya kombe la dunia dhidi ya San Marino na Montenegro
kufuatia kujitokeza tena kwa maumivu yake ya kifundo cha mguu yaliyopelekea
kuwa nje ya uwanja msimu mzima uliopita.
Licha ya vyombo mbalimbali vya habari
kuandika juu ya kurejea kwa kiungi huyo katika hali yake ya kawaida katika wiki
za hivi karibu, bado Wenger anadai kuwa maumivu hayo huenda yakamuweka nje ya uwanja
kwa nyakati tofauti na kwamba kwasasa hajui ni lini atarejea uwanjani.
Meneja huyo mfaransa pia amesema Theo
Walcott, Kieran Gibbs na Abou Diaby huenda wakaungana katika benchi na kiungo
katika mchezo wao wa jumamosi dhidi ya Reading.
XAVI HERNANDES AOMBA KUWA FITI DHIDI YA PSG
Kiungo wa Barcelona Xavi Hernandez amesisitiza
kuwa atakuwa fiti kimchezo katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa robo fainali ya
michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Paris Saint-Germain Jumanne.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Hispania
amekuwa na maumivu ya msuli yaliyopelekea kukosa mazoezi ya leo asubuhi ambapo
amelazimika kufanyiwa matibabu ya kunyoosha misuli (physiotherapy).
Xavi atalazimika kupumzishwa mchezo
wa Jumamosi wa ligi kuu ya nchini Hispania La Liga dhidi ya Celta, huku bado
mashaka yakiwepo kuelekea katika mchezo dhidi ya PSG jijini Paris.
Amenukuliwa akisema
"Sitacheza dhidi ya Celta mwishoni
mwa juma, lakini nitakuwa tayari dhidi ya Paris Saint-Germain,".
Barca iliwakosa Adriano, Jordi Alba,
Carles Puyol na Pedro katika siku za hivi karibuni kufuatia kukabiliwa na
majeruhi.
Trancesco Totti anasema baada ya Messi hakuna kama yeye.
Mshambuliaji mkongwe wa Roma Francesco
Totti amejisifu kuwa ni mshambuliaji mmoja tu aliye na uwezo zaidi yake katika
ulimwengu huu wa soka na huyu si mwingine bali ni Lionel Messi wa Barcelona.
Totti mwenye umri wa miaka 36 ambaye
alikuwa akihusishwa na kurejea katika timu ya taifa kufuatia msimu huu kuwa katika
kiwango cha juu, amesema kuwa Messi ni kiwango kingine lakini ukiachana na
Messi hakuna mwingine zaidi yake.
Akiongea na La Gazzetta dello Sport
Totti amesema kuwa duniani kwasasa kuna mchezaji mmoja tu ambaye anafanya vitu ambavyo
yeye hawezi kufanya ambaye ni Messi na pia hadhani kama nchini Italia kuna
mchezaji kama yeye.
Mshambuliaji huyo mzoefu pia akaenda
mbali zaidi akimpongeza kocha Marcello Lippi , huku pia akisema angependelea baadaye
kufanya kazi na Jose Mourinho.
Totti amemponda mshambuliaji wa AC
Milan Mario Balotelli akisema mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester City bado
si lolote si chochote.
Rooney anasema Engalnd ijifunze kutokana na makosa.
Mshambuliaji wa Manchester United na
timu ya taifa ya England -Wayne Rooney anaamini kuwa England itakuwa imejifunza
kutoka na makosa yaliyo jitokeza katika mchezo uliomalizika kwa sare dhidi ya bao
1-1 dhidi ya Montenegro.
Kikosi cha kocha Roy Hodgson walikuwa
wakiamini kuwa wangeibuka na ushindi katika mchezo huo baada ya bao la mapema
la Rooney kunako dakika ya sita ya mchezo lakini wageni wakafaniwa kusawazisha.
Rooney mwenye umri wa miaka 27
anaamini kuwa kuna haja ya kurejea na kujipanga upya kwa ajili ya michezo
iliyosalia ya kampeni ya kuwania kufuzu fainali ya kombe la dunia ambapo
michezo mitatu kati ya minne iliyobaki italuwa ikichezwa katika uwanja wao wa
nyumbani wa Wembley.
Amenukuliwa akisema
"Bado tuna nafasi kubwa ya
kufuzu, hilo lilikuwa ni somo kwetu hususani katika kipindi cha pili na
tunapaswa kujifunza na kusaka namna ya kufanya vema.
No comments:
Post a Comment