Mlinzi wa
kati wa timu ya Young Africans Ladislaus Mbogo anaendelea vizuri baada ya jana
kufanyiwa upasuaji wa uvimbe (shavuni) katika Hospitali ya Mwananyamala jijini
Dar es salaam, upasuaji uliofanyika chini ya usimamizi wa daktari wa timu ya
Young Africans Dr Nassoro Matuzya.
Mara baada
ya mazoezi ya leo asubuhi katika uwanja wa mabatini Kijitonyama, wachezaji wote
wa Young Africans pamoja na benchi la ufundi waliongozana kwenda Hopsitali ya
Mwananyamala kumpa pole Mbogo ambaye jana alifanyiwa upasuaji wa uvimbe sehemu
ya shavu la kushoto.
Akiongea leo
asubuhi baada ya kutembelewa na wachezaji na benchi la Ufundi, Mbogo amesema
anajisikia vizuri, anamshukuru mungu upasauji umeenda vizuri na hali yake
inaendelea kuimarika hivyo anaamini muda si mrefu atarudi katika hali yake ya
kawaida.
Mbogo ambaye
alisajiliwa mwaka jana katika msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom 2012.2013
akitokea timu ya Toto Africans, amekifikia hatua hiyo ya kukubali kufanyiwa
upasuaji kufuatia kufanyiwa uchuguzi na madakatari kutoka hospital ya
Mwananyamala.
Dr Nassoro
Matuzya akiongea kwa niaba ya madaktari waliomfanyia upasauaji, amesema
upasuaji ulifanikiwa kufanyika salama kabisa, tulimfanyia upasuaji jana asubuhi
kufikia mida ya mchana tayari tulikua tumeshamaliza na kwa sasa yupo wodini kwa
mapumziko chini ya uangalizi wa madakatari.
Kwa mujibu
wa daktari wa Yanga, Dr Matuzya, Mbogo atakua nje ya uwanja kwa kipindi kisichopungua wiki tatu akiendelea kuunguza
sehemu aliyofanyiwa upasuaji.
[Haruna
Niyonzima akiongea na Ladislau Mbogo asubuhi ya leo walipokwenda wachezaji wa
Yanga kumjulia hali hospitali]
Haruna
Niyonzima akiongea na Ladislau Mbogo asubuhi ya leo walipokwenda wachezaji wa
Yanga kumjulia hali hospitali
Katika hatua
nyingine Kikosi cha Young Africans kimeendelea na mazoezi yake katika uwanja wa
mabatini Kijitonyama kujiandaa na mchezo dhidi ya timu ya Ruvu Shooting, mchezo
utakaofanyika siku ya jumamosi katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es
salaam.
Kikosi cha
wachezaji 25 kipo kambini katika hosteli za klabu zilizopo mitaa ya
Twiga/Jangwani ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mchezo huo wa jumamosi,
mchezaji pekee ambaye hayupo kambini ni Ladislasu Mbogo ambaye amedanyiwa upasuaji
wa uvimbe sehemu ya shavuni.
No comments:
Post a Comment