Hii ni baada ya kushuka kwa ununuzi wa hisa za klabu hiyo kwa zaidi ya asilimia tano kwenye soko la hisa la New York.
Wachambuzi wa masuala ya biashara wameeleza hofu
yao juu ya kushuka kwa biashara za United kufuatia kuondoka kwa
Ferguson kwa kusema itakuwa kazi kubwa kumpata mrithi wake ambaye
ataweza kuchagiza mafanikio ya klabu hiyo yatakayovutia wadhamini
mbalimbali kama alivyofanya kwa miaka 27 aliyokaa na United.
Familia ya Malcom Glazer yenye makao yake Miami
nchini Marekani ambayo ndio inayomiliki klabu ya Manchester United bado
haijatangaza mrithi wa Ferguson japo wadadisi na vyanzo vya karibu vya
United vinasema huenda kocha wa Everton, David Moyes akakabidhiwa jukumu
la kuifundisha United,taarifa ambazo hazijathibitishwa wala kukanushwa
na uongozi wa Old Trafford.
Kushuka huko kwa hisa za United kumeifanya klabu
hiyo kupoteza mapato yake kwa karibu asilimia 1.3 kwa hisa moja ambayo
hununuliwa kwa dola za kimarekani 18.52 kwa hisa.
Licha ya kushuka kwa hisa hizo kufuatia taarifa
za kustaafu kwa Ferguson lakini zaidi ya asilimia 30 ya hisa za United
ziliuzwa kwenye soko la hisa hii leo.
No comments:
Post a Comment