Mshambuliaji wa Barcelona raia wa Ajentina Lionel Messi atatakiwa kupanda kizimbani mwezi Septemba kusikiliza kesi dhidi yake ya ukwepaji wa kodi nchini Hispania.
Mshambuliaji
huyo mwenye umri wa miaka 25 ambaye ametajwa mara nne kuwa mchezaji bora wa
dunia pamoja na baba yake Jorge wanakabiliwa na mashitaka ya kukwepa kodi
katika mamlaka za kodi nchini Hispania ya zaidi ya euro milioni 4 sawa na pauni
milioni £3.4m sawa na shilingi bilioni 8.6 za kitanzania.
Inaarifiwa
kuwa Messi aliyatumia makampuni ya huko Belize na Uruguay kuuza haki ya matumizi ya sura
ya Messi.
Mshahara kamili
wa Messi anaolipwa na Barcelona ni euro milioni 16 kwa mwaka na kumfanya kuwa
mchezaji mwenye thamani kubwa zaidi duniani.
Messi ana
mikataba mbalimbali na wadhamini wengi duniani.
Mchezaji huyo
ana mikataba ya kutumia picha yake na makapuni ya Banco Sabadell, Danone,
Adidas, Pepsi-Cola, Proctor and Gamble and the Kuwait Food Company.
Na endapo
atapatikana na hatia basi huenda akaenda jela miaka sita na faini kubwa hii
ikiwa ni kwa mujibu wa shirika la habari la Hispania Efe news agency.
No comments:
Post a Comment