Gareth
Bale amesema hataki kuona nyota mwenzake Cristiano Ronaldo akiondoka Real Madrid
kurudi Uingereza kwenye ligi ya Premier.
Licha
ya Ronaldo kuendelea kufunga mabao ikiwemo matatu wikendi jana dhidi ya
Athletic Bilbao yaliomfanya afikishe rekodi ya ‘hat-trick’ ya 22 katika La Liga
na kufikia rekodi ya ligi iliyowekwa na wachezaji wa zamani Telmo
Zarra na Alfredo Di Stefan.
Ronaldo
amekuwa katika uvumi wa kutaka kurudi katika timu yake ya zamani ya Manchester United msimu ujao wa kiangazi.
Hivi
majuzi, zilizuka tetesi kuwa Ronaldo anaweza kurudi katika timu yake ya zamani
ya United ua Manchester City na Bale ametangaza hataki nyota mwenzake arudi
kwenye ligi ya Premier.
Amedhihirisha
ni mchezaji wa kiwango cha kimataifa amekuwa anafunga mabao mengi.
Bila
shaka, hatutaki aondoke na ninataka asalie hapa Real Madrid,” Bale alisema.
&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&
Luis Suarez apongeza kitendo cha Cavani kutaka kuondoka PSG
Mshambuliaji
wa timu ya Barcelona Luis Suare ameunga mkono kitendo cha
mshambuliaji mwenzake wa timu ya taifa ya Uruguay Edinson Cavani kutaka
kuondoka katika timu ya PSG.
Suarez
amemueleza Cavani anajishusha mwenyewe kwa kukubali kuwa nyuma ya Zlatan Ibranimovic katika timu ya PSG.
Cavani
amekuwa akihusishwa kutaka kwenda kujiunga na timu za Arsenal, Manchester United, Liverpool wiki hii aliyekuwa mshambuliji wa
Liverpool Suarez amesema si kitu
kizuri kuona wanamchezesha Cavan katika nafasi tofauti na nafasi yake.
Paris
imefanya maisha kuwa magumu kwa Cavani ni bora aondoke.
&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&
Mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 27 alijeruhiwa wakati timu hiyo ilipopata ushindi
katika mechi dhidi ya Crystal Palace siku ya jumamosi.
Timu
ya Hull imesema kuwa mchezaji huyo anauguza jeraha la mgongo.
Misri
itachuana na Botswana ugenini siku ya ijumaa na baadaye katika uwanja wa
nyumbani siku tano baadaye huku shinikizo zikizidi dhidi ya Kocha Shawky Gharib
baada ya timu hiyo kushindwa mara mbili katika kundi la G.
Timu
hiyo ya Pharaoh haina pointi hata moja ,pamoja na timu ya Botswana na sasa
inakabiliwa na kibarua kigumu kufuzu katika mechi za AFCON mwakani nchini
Morrocco.
Siku
ya jumanne Rais wa shirikisho la soka nchini Misri Gamal Allam alisema kuwa
kushindwa kwa timu hiyo ya taifa ni jukumu la kamati yake ya kiufundi.
''Tutamuajiri
meneja kutoka nchi za kigeni iwapo Gharib atashindwa kuipeleka timu hiyo katika
fainali za mataifa ya afrika nchini Morocco mwakani alisema Gamal.
&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&
Mchezaji
huyo wa zamani wa kikosi cha Ujerumani ni miongoni mwa watu 22 walioamua ni
wapi kinyang'anyiro hicho cha mwaka 2018 na 2022 kitafanyika katika kura
iliofanyika mnamo mwezi Disemba mwaka 2010.
Akizungumza
katika mkutano wa kuimarisha mchezo huo, mwaka 2014 ,Beckenbauer alikataa
kusema ni nani aliyempigia kura ,ijapokuwa ilidaiwa kuwa alipendelea fainali hizo zifanyike nchini Australia.
''Ilikuwa
ni kura ya siri,nilishangaa kuona Qatar ikiibuka mshindi'',Alisema mchezaji
huyo mkongwe.
Mchezaji
huyo wa zamani ambaye alishinda kombe la dunia kama mchezaji na meneja wa timu
ya Ujerumani ,aliongezea kuwa,ushindani ulikuwa mzuri,kama ile mingine lakini
hakukuwa na tofauti kubwa.
Lazima
kuna sababu kwa nini zile nchi nyengine hazikufanikiwa kuandaa fainali.
Beckernbeur enzi za uchezaji wake |
Qatar
iliishinda Australia,Japan ,korea kusini na Marekani katika kura ya kuandaa fainali
za kombe la dunia mwaka 2022,huku Urusi
ikiishinda Uingereza pamoja na Ubelgiji na Uholanzi,Ureno na Uhispania kwa haki
ya kuandaa kombe la dunia la mwaka 2018.
Ni
kamati kuu ya FIFA ndiyo iliyotoa uamuzi huo ambao umekumbwa na utata tangu
tangazo hilo lifanywe.
Wanachama
wawili wa zamani wa Shirikisho hilo walizuiliwa kushiriki katika kura hiyo
kutokana na madai ya ufisadi,huku wengine sita wakilazimishwa kujiuzulu baada
ya kura hiyo.
Backenbauer
alijiondoa katika kamati hiyo mnamo mwaka 2011.
&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&
NJE YA SOKA NDANI YA CRICKET:
Charlotte Edwards kutoka Uingereza kushiriki katika tuzo za mwaka 2014.
Charlotte Edwards kutoka Uingereza kushiriki katika tuzo za mwaka 2014.
Charlotte Edwards kutoka Uingereza kushiriki katika tuzo za mwaka 2014. |
Baraza
la kimataifa la mchezo wa Cricket limemtaja nahodha wa timu ya taifa ya
wanawake ya mchezo wa Cricket Charlotte
Edwards kutoka Uingereza kushiriki katika tuzo za mwaka 2014.
Edwards,
34, ni mwanamke pekee aliyetajwa katika
orodha ya wachezaji wanaowania tuzo hiyo wengine ni nahodha wa Sri Lanka Angelo
Mathews.
Mitchell
Johnson kutoka Australia, Dale Steyn kutoka Afrika kusini na Huvneshwar Kumar kutoka india.Tuzo
hizo zitapigiwa kura na mashabiki wa mchezo huo kwa njia ya mitandao.
Mshindi
wa tuzo hiyo atatangazwa jumatano ya November 5 Washindi
wa tuzo zilizopita nyota wa India Sachin Tendulkar na Mahendra Dhoni, na kutoka
Sri Lanka Kumar Sangakkara.
&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&
Nafuu nyingine kwa Luis Van Gaal kufuatia kurejea dimbani kwa Michael Carrick
Nafuu ya Luis van Gaal baada ya Carrick kuthibitika kurudi |
Kocha wa Man United Louis Van gaal amesema kiungo wake MICHAEL CARRICK anajiandaa
kurudi dimbani.
Kiungo huyo wa miaka 33 alikuwa nje ya uwanja kutokana na kusumbuliwa
na maumivu ya kifundo cha mguu.
Michael Carrick kurejea uwanjani |
Kukosekana
kwake kumesabisha kuyumba kwa kikosi cha kocha huyo hasa sehemu kiungo cha kati.
Akizungumza
katika mkutano wa waandishi wa habari kocha
Louis amesema kukosekana kwa kiungo huyo mkabaji kulisababisha kutofanya vizuri
na hasa ikizingatiwa ana uzoefu katika soka.
No comments:
Post a Comment