KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, June 19, 2013

Rais wa Brazil kusikiliza kilio cha waandamanaji

Rais Dilna Roussef wa Brazil ameahidi kusikiliza kilio cha waandamanaji ambao wameandamana nchi nzima kupinga gharama kubwa za maandalizi ya michuano ya kombe la Dunia la kandanda.

 Maadamano hayo ni makubwa kabisa kuwahi kushuhudiwa nchini humo katika kipindi cha zaidi ya miaka 20. Roussef aliyapongeza maandamano hayo hapo jana ambapo amesema yameonyesha nguvu ya demokrasia yao, nguvu ya sauti iliyoko mitaani na nguvu ya kiraia ya wananchi wao.
 Katika hotuba yake katika Kasri la Rais amesema kwamba sauti hizo zinapaswa kusikilizwa na kwamba serikali yake inasikiliza sauti hizo zinazodai mabadiliko.

Leo zaidi ya wananchi 200,000 wa Brazil wameingia tena barabarani. Maandamano hayo ambayo kwa kiasi kikubwa yanaongozwa na wanafunzi yalianza yakiwa madogo na yalichochewa na kupanda kwa nauli za usafiri wa umma baadaye kupitia mitandao ya kijamii yaligeuka kuwa vurugu na kulenga gharama kubwa za maandalizi ya michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2014 na Michuano ya Olimpiki ya mwaka 2016.

No comments:

Post a Comment