Guus Hiddink amejiuzulu kazi Anzhi na anatazamiwa kujiunga na Barca.
Guus Hiddink anajipanga kuchukua nafasi ya umeneja katika klabu ya Barcelona baada ya kujiuzulu katika nafasi kutoka katika klabu ya Anzhi Makhachkala.
Klabu tajiri ya Anzhi Makhachkala ua Urusi imetangaza kuwa meneja huyo wa zamani wa Chelsea na Uholanzi ameachia kazi katika klabu hiyo hii leo ikiwa ni taarifa ya ghafla.
Hiddink
ambaye alisaini mkataba wa mwaka mmoja wa nyongeza mwezi Juni amekuwa akikanusha kutaka kufanya kazi na vilabu mbalimbali katika miaka ya hivi karibuni lakini ofa hii ya sasa kutoka katika klabu ya Barcelona imeonekana kuwa ni nono kwa Mduchi huyo.
Suala la kubashiri kwa Hiddink kuchukua nafasi ya Tito
Vilanova ndani ya Nou Camp lilisamimishwa kutoka kwa makampuni mengi ya kubashiri meridiani sports bookmaker ambao ni wadhamni wakubwa wa blog hii muda mfupi baada ya tangazo la kuondoka kwa meneja huyo kutoka katika klabu ya Anzhi.
Katika taarifa kupitia mtandao wa klabu hiyo imesema Hiddink ambaye alisaini mkataba wa mwaka mmoja wa mwezi Juni, imesema,
'Maamuzi haya hayakuwa rahisi kwangu lakini siku zote nitasema kuwa mipango yangu itamalizika wakati klabu itakapo weza kujiendeleza kukuwa yenyewe bila ya ushiriki wangu.
'Sasa wakati umefika. Nashawishika kwamba klabu ina mipango mikubwa ya baadaye, na ninafuraha nilikuwa sehemu mradi mkubwa wa soka.'
Vilanova alijiuzulu katika klabu ya Barca kama bosi wiki iliyopita baada kuwepo katika benchi la ufundi kwa mwaka mmoja ambao aliutumia katika kutibu maradhi yake ya kansa.
Tito Vilanova aliyejiuzulu Barcelona kutokana na kusumbuliwa na kansa
Hiddink atarithi kikosi chenye wakali kama Lionel Messi (kushoto), wakati huu kuna wasiwasi mkubwa juu ya hatma ya Cesc Fabregas ambaye huenda akajiunga na United.
Rene Meulensteen kocha wa zamani wa kikosi cha kwanza cha United anakuwa meneja wa muda wa Anzhi
Hiddink, mwenye umri wa miaka 66, anaonekana kuwa na historia nzuri yenye mafanikio mazuri katika soka la Ulaya yaani CV akiwa amefanya kazi katika bara hilo tangu mwaka 1987.
Aliiongoza Chelsea kushinda taji la FA mwaka 2009 akiwa katika klabu hiyo kwa muda na pia alikuwa katika kipindi cha msimu mmoja katika klabu pinzani ya Barcelona Real Madrid msimu wa 1998-99.
Kocha wa zamani wa kikosi cha kwanza cha Manchester United Rene Meulensteen anakuwa meneja wa muda wa Anzhi.
No comments:
Post a Comment