KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, August 12, 2013

TIMU ZA POLISI TANZANIA ZAAGWA, ZATAKIWA KUJILINDA NA UKIMWI PIA KURUDI NA USHINDI SARPPCO( lenziyamichezo.blogspot.com.

Naibu Kamishina wa Polisi, (DCP) Thobias Andengenye (kushoto) akimpa mkono nahodha wa timu ya Polisi, Makame Ally (kulia) wakati wa hafla ya kuwaaga wachezaji wanaokwenda kwenye mashindano ya polisi kwa nchi zilizopo Kusini mwa jangwa la Sahara (SAPCCO) iliyofanyika Chuo cha Maafisa Polisi, Kilwa road leo.
Wanamichezo wa kiume wakimsikiliza mgeni rasmi.
Wanamichezo waanawake wakimsikiliza mgani rasmi
Naibu Kamishina wa Polisi, (DCP) Thobias Andengenye akizungumza  wakati akiwaaga wanamichezo
Wanamichezo wakiwa pamoja na maofisa wa polisi
WANAMICHEZO wa jeshi la Polisi Tanzania wanaokwenda kwenye michezo ya polisi kwa nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara (SARPPCO) wameagwa leo na Naibu Kamishina wa Polisi, (DCP) Thobias Andengenye na kutahadharishwa kujilinda na ugongwa wa UKIMWI ili waweze kufanya vizuri kwenye michezo hiyo.
Akizungumza kabla ya kukabidhi bendera Naibu Kamishina wa Polisi, (DCP) Thobias Andengenye alisema lengo la michezo hiyo ni kuwafanya wafahamiane na polisi wa nchi zingine pia kubadilishana mbinu za kupambana na uhalifu.

Timu zinazokwenda kwenye mashindano hayo ni soka, mpira wa pete (netboli) darts na riadha ambapo wanamichezo 67 ndio waliokwenda.

No comments:

Post a Comment