Meneja wa Arsenal Arsene Wenger anataka kumsajili mchezaji wa Borussia Monchengladbach Patrick Herrmann.
Bosi huyo wa washika mitutu ametenga pesa ya kutosha katika uwekezaji wa wachezaji hususaani kwa wachezaji wa kutoka nchini Ujerumani ambapo katika miaka ya hivi karibuni wamekuwa wakichukua vipaji kadhaa kama vile Per Mertesacker, Lukas Podolski, Serge
Gnabry na Mesut Ozil.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 22 pia amekuwa akihusishwa na kutaka kuelekea katika vilabu vya Barcelona na
Liverpool, kwani kwasasa amekuwa nyota mkubwa katika soka la ligi ya Bundesliga na Arsenal wakionekana kujipanga na kudaka saini yake.
No comments:
Post a Comment