Misri haitamfukuza kocha wake Bob Bradley baada ya kichapo cha jana cha mabao 6-1 kutoka kwa Ghana mjini Kumasi ukiwa ni mchezo muhimu wa kusaka tiketi ya kucheza kombe la dunia kabla ya mchezo wa marudiano mwezi Novemba.
Taarifa za awali ziliarifu kuwa kocha huyo mmarekani huenda angefukuzwa kazi kufuatia matokeo hayo mabaya kabisa katika historia ya soka ya nchi hiyo katika michezo ya kimashindano kusaka nafasi ya kucheza kombe la dunia nchini Brazil Mwakani.
Endapo Misri itamfukuza kocha huyo italazimika kumlipa kisai cha dolari za kimarekani US$366,000 kama fidia ya kukatisha mkataba.
Chama cha soka cha Misri EFA kupitia kwa mwenyekiti wake Gamal Allam
kimesema
"Haiingi akilini kumfukuza na kumlipa kabla ya mchezo wa mwisho ndani ya mkataba wake."
Lakini katika hatua nyingine FA ya Misri inaangalia uwezekano wa kocha msaidizi Diaa El Sayed kuchukua nafasi katika benchi la ufundi ( katika dugout) Novemba 19 katika mchezo wa pili wa marudiano kwa kuhofia usalama wa Bradley.
Kichapo kisicho vumilika kutoka kwa Ghana kimewaja hasira mashabikiwa wa Misri na polisi walilazimika kuongeza usalama katika uwanja wa ndege asubuhi ya leo wakati kikosi cha Misri kikirejea.
Allam anaamini mashabiki wenye hasira wasingependelea kumuona Bradley akiruhusiwa kuongoza kikosi katika mchezo wa pili.
Siku mbili zilizopita Polisi walikabiliana na kundi la mashabiki la Ahly Ultras, ambao walitaka kujaribu kuivamia timu ya mchezo wa mikono ya Ahly
baada ya kuchapwa katika michuano ya kusaka ubingwa ya "Champions
Handball League" na timu ya nchini Tunisia.
No comments:
Post a Comment