Nyumba ya England nchini Brazil: England itaweka maskani katika hoteli hii ya Royal Tulip Sao Conrado Beach Hotel mjini Rio de Janeiro wakati wa fainali ya kombe la dunia.
Pahala pa kulala: vyumba vya Royal Tulip ambako Roy Hodgson na kikosi chake wataweka kambi.
Sehemu ya maakuli
Sehemu ya mapumziko.
Kikosi cha meneja Roy Hodgson kitakuwa kambini nchini Brazil katika hoteli ya nyota tano ya Royal Tulip Hotel mjini Rio de Janeiro wakati wote wa michuano ya kombe la duni ambayo inatarajiwa kuanza mwezi Juni.
Hoteli hiyo ina jumla ya vyumba 418 ndani ya ghorofa 17 sehemu ya mapumziko ya wazi yenye kukuwezesha kuona ufukwe wa Sao Conrado Beach au Gavea Stone.
Baada ya kufanikiwa kupata nafasi ya kufuzu baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Poland, wakuu wa FA hawakuwa na muda wa kupoteza kwa kusaka nafasi ya kikosi huko nchini Brazil.
Katibu mkuu wa FA Alex Horne amekiambia kituo cha Sky Sports News kuwa
'Dro itafaniyika mpaka Desemba 6 lakini tumesha fanya mipango tayari tumejadiliana na FIFA juu wa wapi tutakwenda kukaa.
'Unatakiwa kuwa na mipango ya mbele kwanza juu ya hili, FIFA inateua hoteli na viwanja vua mazoezi na sisi tumefanya kazi yetu na tumechagua wapi tunakwenda kuweka kambi yetu nchini Brazil na itakuwa katika jiji la Rio.'
Katibu mkuu wa FA Alex Horne amekiambia kituo cha Sky Sports News kuwa
'Dro itafaniyika mpaka Desemba 6 lakini tumesha fanya mipango tayari tumejadiliana na FIFA juu wa wapi tutakwenda kukaa.
FA imeichagua Royal Tulip baada ya mipango kuwekwa wazi kwa fanzone nje ya Windsor Atlantica huko Copacabana Beach.
Lakini hoteli iliyopendekezwa haina kiwango kinachotakiwa lazima kazi kidogo ifanyike ya marekebisho ili kufikia kiwango cha timu ya England.
Ina hadhi ya hoteli ya 97 kati ya hoteli 204 za Rio baada ya kupitia mtandao wa TripAdvisor.
Miundo mbinu ya uwanja wa mazoezi wa Urca Military base, ambao England itafaanya mazoezi kunahitaji kufanyiwa kazi.
No comments:
Post a Comment