KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, October 16, 2013

Claudio Ranieri awapiga mkwara Chelsea na Real Madrid kuwa thamani ya Falcao ni zaidi ya Bale. Soma...............

Kocha wa klabu ya Monaco ya nchini Ufaransa Claudio Ranieri amewaonya Chelsea na Real Madrid kwamba Radamel Falcao atawagharimu kiasi cha pauni milioni £168 endapo kweli watakuwa wakimtaka wakati wa uhamisho wa dirisha la usajili la mwezi Januari
Falcao, ambaye alikuwa pekee aliyejiunga na Monaco wakati wa uhamisho wa Kiangazi anabaki windo pekee la Jose Mourinho huku Real Madri nao wiki hii wakithibitisha kuwa wanamtaka mshambuliaji huyo.

Amenukuliwa Ranieri akisema,
Kama Gareth Bale anathamani ya euro milioni €100, vipi kuhusu Falcao? atakuwa euro milioni €200 ambazo ni sawa na pauni milioni £168,’.
Falcao ameonekana kung'ara akiwa na Monaco tangu ajiunge nao mwezi Mei baada ya kufunga jumla ya magoli saba katika michezo ya mwanzo saba na kukiweka kikosi chake katika usukani wa ligi ya Ufaransa maarufu kama Ligue 1.
Taarifa za hivi karibu kutoka nchini Ufaransa zinaeleza kuwa mshambuliaji huyo raia wa Colombia hana furaha na maisha yake ndani ya klabu hiyo na yuko katika mpango wa kuondoka mwezi Januari.
Chelsea imekuwa na mpango wa kunasa huduma ya Falcao kwa zaidi ya miezi 18 na imemuweka katika orodha ya wachezaji watatu wanaotakiwa na klabu hiyo wakati wa mwaka mpya huku Madrid wakionekana kuweka upinzani mkubwa wa kumsajili lakini wakisubiri mpaka kiangazi ijayo.

No comments:

Post a Comment