KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, October 2, 2013

Ferguson asema hatarudi ulingoni.

Meneja wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson amesisitiza kuwa hatarejea katika shughuli za ukocha wa soka.
 Manchester United hivi sasa wanashikilia nafasi ya 12 katika Ligi Kuu ya England chini ya uongozi wa David Moyes, aliyeshikilia nafasi hiyo baada ya Ferguson kustaafu mwishoni mwa msimu uliopita.
 "Mimi sina hamu ya kuwa meneja tena ,na kujisumbua roho yangu ," alisema Ferguson. "United wako mikononi mwa uongozi mzuri. David atakua poa. Ni meneja mzuri."
Ferguson, mwenye umri wa miaka 71,alidokeza kwamba Roman Abramovich alimtaka aiongoze Chelsea alipoinunua mnamo mwaka 2003.
"walimtuma wakala aniulize Abramovich alipochukua madaraka kwa mara ya kwanza ya klabu hiyo lakini niliwaambia 'Ng'oo."

No comments:

Post a Comment