UCHAGUZI
WA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF) 2013ILANI YANGU YA UCHAGUZI
Utangulizi
Ndugu
zangu,
Nianze kwa
kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema aliyetulinda na kutuwezesha
kufikahapa tulipo.
Tarehe 19
Novemba 2009 Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati anazindua ziara ya Kombe la FIFA
la dunia uwanja wa Taifa, Dar Es Salaam pamoja na mambo mengine alisema,
namnukuu:
‘‘Kwa
Watanzania wenzangu tuichukulie ziara ya Kombe la Dunia nchini mwetukama ni changamoto
kubwa kwetu inayotutaka tufanye vizuri zaidi katika soka ilitulingane na
heshima hii tuliyopewa.
Hasa ni
changamoto kwa viongozi wa soka wangazi zote pamoja na wachezaji na wapenzi wa
mpira wa miguu nchini. Kuja kwakombe hili ni deni kwetu na kulilipa kwetu sisi
ni kuzinduka, tuendeleze kiwangochetu cha soka nchini ili na sisi siku moja.
TUSHIRIKI
FAINALI ZA
KOMBE HILI.
(Msisitizo
ni wa kwangu). Hili jambo linawezekana. Wapo wenzetu Afrika wameweza, kwa nini sisi
tusiweze? Wao ni watu kama sisi, maadam wameweza nasisi tutaweza.Lakini ili
tuweze hatuna budi kuiga mfano hususani waliyofanya wenzetu na wanayoendelea kufanya
kuendeleza mpira wa miguu.
Twende
tukajifunze kutoka kwao. Lakini hata kabla
ya kwenda huko, yapo mambo hatuna budi kuyafanya. Naomba nitaje
baadhi yake:
1.Tuimarishe
Uongozi, utendaji na uendeshaji wa vilabu vya mpira. Mchezaji hufundishwa kucheza
mpira katika Klabu yake. Hapo ndipo hufundishwa maarifa ya kucheza mpira na vipaji
kuendelezwa.
Hebu tujiulize
hali ya vilabu vyetu vya soka ikoje. Je vinaongozwa vizuri? Vinaendeshwa vizuri?
Jibu tunalijua sote kuwa ni hapana. Lazima suala hili tulitafakari kwa makinina
kulipatia jawabu. Tukishindwa kupata jawabu muafaka na mambo yakaachwa
kuendelea yalivyo, mpaka mwisho wa dunia hatutakuwa tunasogea popote.
2. Tupate
walimu wenye uzoefu kufundisha timu zetu. Hii ndiyo njia ya uhakika ya kukuza
na kuendeleza vipaji na hivyo kupata wachezaji bora.
3. Tuwekeze
katika kuibua na kuendeleza vipaji vya wachezaji toka umri mdogo.Vilabu viwe na
timu za watoto na vijana. TFF isaidie kuanzishwa kwa shule za mchezo wa mpira
wa miguu kwa watoto na vijana. Mashuleni wapatikane walimu wa michezo walio
wazuri kufundisha.
4. TFF
ionekane zaidi ya ilivyo sasa katika mipango ya kuendeleza soka mashuleni,
vijijini, mitaani na vilabuni. TFF ikiwa na mipango na kuisimamiana kuwabana wadau
kuitekeleza itasaidia. Vinginevyo TFF itabakia kusimamia Ligi Kuu, kutoa adhabu
kwa wachezaji na kusimamia timu yaTaifa. Hiyo haitoshi.’’
Mwisho wa
kunukuu.
Ndugu
zangu wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF, wadau na wapenzi wa mpira wa Miguu
Tanzania tujiulize kuanzia kipindi hicho cha 2009 hadi leo hii katika haya
maagizo ya Mheshimiwa Rais JakayaMrisho Kikwete tumetekeleza yapi zaidi ya kuwa
wasindikizaji katika medani ya kimataifa?
Kipindi chote
cha miaka minane iliyopita Serikali imetoa sapoti kubwa katika sekta ya mpira
wa miguu kwa kulipia walimu wa timu za Taifa na kuhimiza makampuni kama NMB, Serengeti
Breweries, Airtel, CocaCola na sasa Tanzania Breweries kudhamini timu zetu za
taifa na mashindano mbali mbali, matunda yake yako wapi? Ndo kwanza tunazidi
kuporomoka kwenye viwango vya FIFA.
Iweje
miaka ya nyuma timu zetu za Taifa zilifanya vizuri wakati zinaweka kambi
Salvation Army, leo zinakaa hotel za nyota tatu mafanikio mbona hatuyaoni?
Kama
TFF imeondolewa gharama za kulipa makocha, kuweka timu kambini, kununua vifaa
vya timu, dawa, posho, malazi pamoja na usafiri wa timu iweje leo TFF ishindwe
kutumia vyanzo vyake vya mapato zikiwemo fedha toka FIFA na CAF kwa ajili
yakuanzisha na kuendeleza programmu ya vijana ya kitaifa?
Kwa mujibu wa mtandao
wa FIFA kati ya mwaka 2008 na 2012 TFF imepokea toka FIFA msaada wa jumla ya
dola za kimarekani milioni moja na lake nane na nusu (yapata shilingi bilioni
tatu za kitanzania), hizi fedha zimefanyia nini?
Kwa nini timu za vijana hazina
udhamini? Ipi timu yetu ya taifa iwe ya wanaume wakubwa (senior team) ,wanawake
au za vijana inayoweza leo hii kujivunia mafanikio?
Iko wapi ligi ya wanawake?
Katika hili tusilaumu Chama cha mpira cha wanawake, wakiwezeshwa
wanaweza.Tutapataje timu mahiri yaTwiga stars bila ligi ya wanawake?
Katika
ngazi ya klabu, hasa zinazoendeshwa kwa mfumo wa kijamii kama Toto Africa,
Coastal Union, Yanga, Simba, Mbeya City n.k. hadi leo hii pamoja na rasilimali
za vilabu hivi ni klabu ipi imeweza kusimamia na kujiendesha yenyewe tokana na
vyanzo vyake yenyewe? Tuendelee kujiuliza:
Ni walimu
wangapi wa mpira tumewaendeleza kufikia kiwango cha kukabidhiwa majukumu yakufundisha
Taifa Stars. Fursa za mafunzo tunazopewa na FIFA na CAF tunazitumiaje? Je tumeweza
kuwa na angalau kocha mmoja anayefundisha mpira nje ya nchi kama ilivyo kwa akina
Sam Timbe ( wa Uganda), James Sianga ( wa Kenya) Jack Chamangwana ( wa Malawi) na
wengine ambao waliweza kufundisha mpira Tanzania kwa ufanisi?
Ni refa
gani tumemuendeleza akafikia kiwango cha kuchezesha mashindano ya fainali za
dunia au AFCON au Klabu bingwa ya Africa? Refa wa mwisho kuchezesha fainali za
Mataifa Africa(AFCON) ni Omar Abdulkadir huko Burkina Faso mwaka 1998.
Ni program
ipi ya vijana ya kuibua vipaji na kuviendeleza tuliyo nayo? Wale vijana wa CopaCocacola
2007 waliopelekwa kwa mbwembwe Brazil waliishia wapi? Tuna rekodi zao? Tunajua
wako wapi na wanafanya nini? Na hawa walioshinda majuzi Afrika Airtel Rising Stars
tumewatangenezea program gani ya maendeleo?
Tunaelewa
matatizo ya vilabu vya mpira hususani uhaba wa vifaa na pesa za uendeshaji, je vilabu
vyetu TFF inavisaidiaje katika kuendeleza programu zao za vijana? Au kazi yetu
ni kudai kila klabu iwe na timu ya under 20 bila kujali gharama za uendeshaji
wa timu hizi?
TFF hadi
sasa imebuni, kusimamia na kutekeleza program endelevu ipi ya kuendeleza soka mashuleni,
vijijini, mitaani au vilabuni? Au mpaka tusubiri Airtel rising Star na CopaCocacola?
Siku wakubwa hawa wakisusa itakuwaje?
Ziko wapi
juhudi za kuhimiza upatikani wa vifaa vya kufundishia mpira watoto (kama mipira
size 3/4) pamoja na kuimarisha miradi ya kuendeleza vijana ?
Hivi timu
zetu za Taifa zinatumia mfumo upi wa uchezaji? Au kila kocha wa taifa
tunayemleta anakuja na mfumo wake? Wenzetu wameweza kubuni mifumo ya uchezaji
ya timu zao zaTaifa na wame ushirikisha katika mfumo wa ufundishaji wa watoto.
Lini Mwalimu
wetu waTaifa alikaa na walimu wa vilabu (angalau vya Premier League) ili
kujadili ufundishwaji wa mpira nchini, hii ikiwa ni pamoja na kujadili masuala
yahusuyo mbinu, lishe, huduma za afyana ukakamavu wa mwili? Hivi mchezaji
akitoka katika klabu yake ambako amezoea kula donana maharage ukampeleka kambi
ya Timu ya Taifa akapewa prawns ,kuku na samaki kwa siku nne za kambi
itamsaidia kumbadili siha? Ng’ombe hanenepeshwi siku ya mnada.Uratibu wa programu
za vilabu ni muhimu.
Raha ya
mpira ni kelele na hoi hoi za mashabiki. Wataalam wa mpira wanasema umoja wamashabiki
wa mpira ni sawa na mchezaji wa 12 uwanjani. Zipo timu ambazo kihistoria zilikuwa
ni za kijamii na zilihamasisha sana ligi ya Taifa, na kuiongeza hamasa na ushindani,
Mbeya City ni mashahidi.
Leo hii
ziko wapi timu kama Ushirika ya Moshi, Bandariya Mtwara, Kariakoo Lindi, Balimi
Bukoba, Reli Kiboko ya vigogo, Kahama United, Mirambo ya Tabora, Tukuyu Stars,
Nyota Korogwe, African Sports ya Tanga, Ujenzi Rukwa, MjiMpwapwa n.k. TFF
imefanya juhudi gani kufufua ushidani huu kwa kushirikiana na vyamavya Mikoa na
Wilaya?
Wapo
wachezaji wastaafu waliojitolea kwa moyo mmoja kuiletea heshima nchi yetu. Leo
hii tunasikia kina Alfonce Modest na Jellah Mtagwa wanalalamika hawana msaada,
na hao ndio wale waliojitolea hadharani kutoa kilio chao. TFF hadi leo hii imewahi
kuandaa mpango gani endelevu wa
kuwasaidia wachezaji wastaafu?
Shirikisho la mpira barani Afrika CAF wameanzisha
ISSA HAYATOU TRUST FUND kusaidia wachezaji wastaafu waishio katika mazingira
magumu, sisi tumechukua hatua gani katika hili?
Iweje mpake leo hakuna mashindano
yoyote ya wanawake ya kitaifa yawe ya ligi au yamtoano,angalau kwa ngazi ya
kanda ? TFF itawezaje kuibua vipaji vipya vya timu ya taifa yawanawake TWIGA
Stars bila mashindano ya aina hii?
Vilabu vya mpira, hususani vya Ligi
Kuu, vimegeuka kuwa kisima cha watu kuchota fedha. Haiyumkiniki vilabu ambavyo
vinaweka timu kambini, kuihudumai kuanzia malazi, posho,vifaa, madawa na
usafiri mwisho wa mechi jumla ya pesa wanayopewa inakuwa chini ya nusuya mapato
yote ya mechi.
Hayo maendeleo ya mpira ambayo yametakiwa yaanzie ngazi yavilabu
yatapatikanaje? Vilabu vimegeuka vitega uchumi vya watu wengine wakati
vyenyewe vinataabika na kujiendesha kwa mateso makubwa.
Ya kusema ni mengi, kwa
leo tuishie hapa.
Nini matokeo ya hali hii? Takwimu
hazidanganyi. Matokeo ya hali hii ni timu za Taifa kushuka viwango katika
orodha ya FIFA siku hadi siku. Viwango vya timu za taifa vinapimwa kwa
kuangalia uwiano wa matokeo ya timu ya wakubwa (senior) pamoja na yale ya timu
nyingine za vijana za nchi husika.
Miaka ya mwanzo ya tisini tulishawahi
kupanda hadi nafasi ya 65, leo hii kila kukicha tuko kwenye 120.
Kuporomoka huku kutaendelea hadi
lini? Ndugu zangu, tujiulize wapi tumetoka, tuko wapi na tunataka kuelekea
wapi? Jibu ni rahisi, kamaalivyoagiza Mh Rais Kikwete,tujipange upya, tubuni
mkakati wa uendelezaji wa mpira, tuandae program endelevu yenye malengo
yanayopimika na kwa pamoja tukishirikiana na Serikali, FIFA, CAF na CECAFA, Halmashauri,
Taasisi zisizo za kiserikali, Sekta binafsi, Vyombo vya habari na wadau wengine
wote wa mpira wa miguu tutaweza kufanya vizuri na kuifanya Tanzania
isifikeduniani kote. Katika kutimiza azma hii sharti tuanzie kwa kuleta.
mabadiliko
ya uongozi wa juu waTFF, tupate
kiongozi ambaye sio sehemu ya mapungufu ya TFF, hakuna njia ya mkato.
Mimi Jamal Emil Malinzi, nimejipima
na ninaamini nina uwezo wa kutosha wa kubuni, kuratibu nakusimamia mabadiliko
haya nikiwa Rais wa TFF.
Ndugu zangu, siku zote si vyema
kukosoa bila kueleza njia mbadala ya kufuata ili kutatua tatizo.
Hapatunazungumzia mpira wa miguu na namna ya kuunasua toka kwenye janga la
kushuka kiwango natimu zetu za Taifa kuendelea kugeuzwa kichwa cha mwenda
wazimu ambacho hadi majuzi vibonde Gambia wamejifunzia kunyoa. Ili tuweze
kuukwamua mpira wetu ni vyema tukakumbushana kuwa ili mpira uendelee unahitaji
vituvinne:
1.Vipaji;
2.Walimu;
3.Vifaa;
4.Viwanja
1.Vipaji
Tanzania ni nchi yenye watu zaidi ya
milioni 44. Nchi ya Cape Verde yenye watu 500,000 tuimeweza pamoja na uchache
wake kuvumbua vijana 11 ambao wameweza kuifikisha nchi yao fainali za Africa
2013 Afrika Kusini na majuzi nusura waende kombe la dunia kama sio tatizo la
utunzaji kumbukumbu. Sayansi ya uibuaji vipaji (scouting) ni muhimu na si kila
mtuanaijua. Watafutwe wanaoijua, watufanyie kazi ya kutuibulia vipaji vipya, na
katika hili nisharti mpira wa ushindani uchezwe nchini kote ili vipaji
vionekane.
2.Walimu
Mpira ni sayansi,mpira ni taaluma.
Kipaji bila mwalimu wa kukiendeleza ni bure. Vijanampira wanaanza kuucheza
wakiwa wadogo hususani wakiwa shule za msingi. Huko ndikoTaifa linahitaji
kusambaza walimu wenye taaluma ya kufundisha mpira ngazi ya awali.Wakishakuzwa
kimpira ni lazima wawepo walimu wa kutosha kuwaendeleza ngazi yawakubwa na
Taifa. Leo hii Uingereza ina walimu 1100 wenye leseni daraja A, Ujerumani
wapo5500 na Hispania 12,000,Tanzania tunaye mmoja tu,kwa mtaji huu tutafika
kweli?Kwa mujibuwa ripoti ya TFF nchi nzima ya Tanzania ina walimu wa mpira wa
madaraja yote elfu mbili tuna mia tano kati yao wako Dar es salaam. Hawa walimu
2000 ndio wanategemewawawafundishe mpira vijana wa Kitanzania zaidi ya milioni
kumi walio katika umri wakufundishwa mpira!
3.Vifaa
Wachezaji, walimu wa mpira, madaktari
na waamuzi wote wanahitaji vifaa vya msingi ilimpira uchezwe. Nchini mwetu
vijana walio wengi wanacheza pekupeku, jezi ni upande mmoja kucheza kifua wazi,
mpira ni wa kuviringisha matambara, refa anavaa suruali, filimbi ni
mluzi, magoli hayana nyavu, n.k.
Hii ndiyo hali halisi ya uchezwaji wa mpira
maeneo mengi Tanzania hasa vijijini ambako ndiko kunapaswa kuwa chimbuko kubwa
la vipaji. Gharama za vifaa vya michezo ziko juu mno, mfano mpira mzuri unaofaa
kuchezewa kwenye ardhi ngumu (rough surface) bei yake ni shilingi laki tatu,
shule ipi ya msingi itawezakuununua huu mpira?
Kuna baadhi ya vyombo vya habari
majuzi viliripoti kuwa kunamchezaji alifunga hat trick ngazi ya Ligi Taifa
akanyimwa mpira kisa ni wa thamani kubwa. Mamlaka husika, hasa za kodi zinapaswa
kuliangalia hili, ili upatikane unafuu katika bei zavifaa vya michezo maana
karibia vyote vinaagizwa toka nje. Lakini pia vifaa vya michezo vyamisaada
vinavyopatikana kutokana na miradi mbalimbali ya TFF ni juu ya TFF
kuhakikishavinafikishwa vijijini pia kupitia vyama vya mikoa na wilaya.
4. Viwanja
Wilayani Ngara mkoani Kagera kuna
uwanja wa mpira unaitwa ‘’Uwanja wa Changarawe’’ na ni kweli uwanja huo umejaa
changarawe. Beki akikaba kwa mtindo wa kuteleza ardhini ‘sliding tackle’ basi
nyama ya paja anaiacha pale chini. Hii ndiyo hali halisi ya viwanja vyetu vingi
nchini, kama viponi vibovu sana maana maeneo mengi viwanja vya mpira hakuna
vimechukuliwa na wajanja wachachena kugeuzwa makazi na majengo ya biashara.
Tunahitaji viwanja vyenye ubora ili vijana wetuwafundishwe mpira wa kisasa kwa
ufanisi, mpira wa kupiga pasi ya chini. TFF kwa kushirikiana navyama vya Mikoa
na Wilaya sharti wawe mstari wa mbele katika kulipigania hili.
1. TFF inatengeneza utaratibu mzuri wa
kuuza bidhaa zake ndani na nje ya nchi kwa kupitia uuzaji wa kawaida na wa
mtandao. Mikataba itaandaliwa ili kudhibiti uuzwaji holela wa bidhaa za TFF.
2.Vyumba vya Maduka vinajengwa
kuzunguka uwanja wa Karume na kukodishwa.
3. Jengo la kitega cha uchumi
litajengwa kwenye ardhi ya Uwanja wa Karume. Pia jukwaa la watazamaji litajengwa
uwanja wa Karume ili mechi ambazo sio kubwa ziweze kufanyika pale, hii
itaviongezea vilabu mapato.
4. Juhudi za kuboresha ukusanyaji,
usimamizi na mgawanyo wa haki wa mapato ya milango ni yatokanayo na ligi yetu
utaboreshwa ikiwa ni pamoja na kubuni vyanzo vipya kupitia njia mbali mbali
zikiwemo za udhamini mbadala kwa vilabu. Aidha jitihada ambazo tayari zimekwisha
anza za kuunda bodi ya kuendesha ligi na uanzishwaji wa utaratibu huru
wakuendesha ligi zitaendelezwa ili kuongeza ufanisi, kuinua mapato ya vilabu na
kuongeza msisimko wa ligi. Ninaunga mkono juhudi hizi.
5. Viwanja vingi vya mpira nchini
vinamilikiwa aidha na Halmashauri, Serikali kuu au vyama vya siasa. Viwanja
hivi vingi viko katika hali mbaya kuanzia nyasi ,hali ya uzio,vyumba vya
kubadilishia nguo, mageti, vifaa vya kuzimia moto n.k. Ni vyema TFF na vyama
vya mikoa kwa kupitia utaratibu wa PPP (Public Private Sector Partnership)
vikaingia ubia na wamiliki wa viwanja hivi ili TFF nawashirika wake wachukue
jukumu la kuviboresha, kuvisimamia na kuviendesha ilikuhakikisha vinakuwa
katika viwango stahili kwa mujibu wa kanuni za FIFA naCAF. Hii itaongeza
usalama wa wachezaji na watazamaji na kuinua mapatoyatokanayo na viwanja hivi
Ushiriki wa wadau Kwa sasa taswira ya
mpira wa miguu inawafungia nje wadau wengi ambao kama wangepewa fursa ya
kushiriki nao wangetaka wachangie maendeleo ya mpira wa miguu. Juhudi kubwa
inabidi zitumike kurudisha imani hii ili kuleta hisia za umoja wa kitaifa
katika kuendesha mpira wetu (sense of
belongingness) . Ni muhimu taasisi muhimu za kitaifa zishirikishwe
katika sekta hii ya mpira wamiguu, hii ni pamoja na taasisi kama
Tacaids,Mashirika ya utalii kama TANAPA na TTB, Umoja wa wafanyabiashara kama
TPSF, CTI na TCCIA ,Kituo cha uwekezaji TIC n.k.Ushirikiano huu
utasaidia kujenga jina la Tanzania pale tunapoandaa michuano ya kimataifa na pia
kuhamasisha vijana wetu waepuke maisha hatarishi kama vile kujihusisha na ngono
isiyokuwa salama,madawa ya kulewa(kutumia na kusafirisha), ulevi wa kupindukia
n.k.
AHADI YANGU
Endapo nitachaguliwa kuwa Rais wa
TFF, kwa kushirikiana na viongozi wote wa TFF kuanzia ngaziya vilabu, Wilaya,
Mikoa na Kamati ya Utendaji Taifa na kwa kuhusisha kwa karibu Vyama
vyakimataifa vya FIFA na CAF, Serikali, Halmashauri,Taasisi zisizo za
kiserikali, Vyombo vya habari,Sekta binafsi, Mashirika ya umma na wadau wa
mpira wa miguu Tanzania ninaahidi kuenzi mafanikioya awamu inayomaliza muda
wake , kustawisha utulivu katika uendeshaji wa mpira, na kufanya jitihada za
kubuni, kuboresha na kustawisha maendeleo ya mpira wa miguu Tanzania. Jitihada
kubwazitawekwa kwenye maeneo makuu yafuatayo:
1.
Ufundi (Technical)
1.1 Muundo wa Idara ya UfundiKatiba
ya TFF imeainisha wazi kuwa TFF ndiye msimamizi mkuu wa mpira wa miguuTanzania,
hivyo jukumu la kuleta maendeleo ya mchezo huu kwa kiasi kikubwa
linaiangukiaTFF.Ni kwa msingi huu basi asilimia kubwa ya rasilimali za TFF
lazima iwekezwe katikakuleta maendeleo ya mpira. Kwa mfumo wetu wa uendeshaji,
kichocheo kikuu cha maendeleoya mpira ni idara ya ufundi ya TFF. Hivyo idara
hii ya ufundi inapaswa kuwa ndiyo idaramama ya TFF ambayo inapaswa kuongoza kwa
matumizi ya fedha, idadi ya waajiriwa namatumizi ya rasilimali nyingine za TFF
. Kwa sasa pale TFF hali sivyo ilivyo. Iwaponitachaguliwa nitapendekeza jukumu
la kwanza la Kamati ya utendaji liwe ni kurekebisha nakuboresha mfumo wa
uendeshaji wa idara ya ufundi. Nitapendekeza idara ya ufundi iendeleekuongozwa
na Mkurugenzi wa Ufundi na chini yake awe na wakurugenzi wasaidizi wa
vitengowatatu Mkurugenzi Msaidizi (ufundi), Mkurugenzi Msaidizi (Elimu na
Mafunzo) ambaye kwasasa anaitwa Education officer, na Mkurugenzi Msaidizi
(Maendeleo ya mpira).
Kitengo cha Ufundi kitahusika na
kubuni na kusimamia shughuli zote zinazohusu maendeleo ya Timu za Taifa kuanzia
za wakubwa hadi za vijana. Hii itakuwa ni pamoja na kuandaa mitaala ya taifa
(national football curriculum) ya ufundishaji wa mpira Tanzania kuanzia umri wa
miaka mitano hadi watu wazima.
Walimu wa Timu za Taifa wataripoti kwake. Kitengo
cha Elimu na Mafunzo kitahusika na kubuni na kuratibu kozi zote na mafunzo
yoteyanayohusiana na mpira kama vile kozi za Marefa, Makocha, Madaktari,
Makamisaa,Watawala, Waandishi wa Habari za Michezo, n.k.
Kitengo cha Maendeleo
ya mpira kitahusika na kubuni,kuratibu na kusimamia mpango wamaendeleo ya
vijana (grassroot) na kutafuta vipaji (scouting). Kitengo hiki kitafanya kazi
kwa kushirikiana kwa ukaribu na idara za Serikali hasa idara za Elimu,Vijana na
TAMISEMI,Halmashauri,Mashirika ya umma,Sekta binafsi pamoja na Taasisi nyingine
za kijamii.
Wakuu wa vitengo hivi wataajiriwa kwa kufuata vigezo makini na bila
upendeleo walakujuana.1.2
Ujenzi wa Kituo cha Mpira (Football
Centre of excellency)Hiki ni Kituo Maalum cha mafunzo ya mpira wa miguu. Katika
kituo hiki kunakuwa na kilaaina ya miundo mbinu, viwanja vya kufundishia mpira,
vituo vya tiba,madarasa ,maabara zautafiti,hosteli n.k Kituo hiki pia kinakuwa
ndio sehemu kuu ya kuweka kambi za timu za Taifana kutoa mafunzo ya ufundi
yakiwemo ya ukocha, urefa, utawala na tiba.
Wenzetu wa Senegal na Ethiopia kwa
kushirikiana na Shirikisho la Mpira Africa CAF wameweza kujenga vituo hivi na
matokeo yake tunayaona. Cameroon pia wana kituo hiki. Pamoja na gharama zake kuwa
kubwa, cha muhimu hapa ni kuweka nia, kutafuta ardhi kwakushirikiana na
Serikali na kuanza ujenzi taratibu. Kwa kuwa klabu ya Sunderland ya Uingereza na
kampuni ya kufua umeme ya Symbion wameonyesha nia ya kushirikiana na Serikali
kujenga kituo cha michezo itakuwa vyema iwapo TFF itashirikiana na taasisi hizi
muhimu ili kufikia azma ya kujenga kituo hiki cha kisasa.
Iwapo nitachaguliwa
nitasimamia uanzishwaji wa mradihuu muhimu ikiwa ni sehemu ya mkakati wa
kulikomboa soka letu.Aidha uwanja wa Karume yalipo makao makuu ya TFF
utazungushiwa jukwaa ili mechiambazo sio kubwa zifanyike pale, Hii itaiongezea
TFF mapato na vilabu pia.
1.3 Timu Kupanda Daraja Ili kuongeza
ushindani na kupanua mpira uchezwe kona zote za nchini ( to spread the
game), mtindo wa kucheza kikanda ili kupata timu za kupanda daraja kuu utakuwa
ni wa kudumu na utaimarishwa kwa kutafutiwa udhamini na kuboreshwa viwanja kwa
kushirikiana na wamiliki
wa viwanja hivyo.
Usimamizi wa
mashindano ngazi hii utaimarishwa na kusimamiwa kwakaribu zaidi ili timu
itakayopanda daraja iwe imepanda kwa haki na hivyo kuleta ushindani Ligi
Kuu.
Hata hivyo waraka uliotolewa na TFF ukiagiza mikoa ichezeshe ligi ili
kupata bingwa wamkoa utafutwa kwa sababu hautekelezeki kutokana na hali ya
uchumi na uhalisia wa jiografia ya mikoa ya Tanzania.
Mathalani Mkoa wa Mtwara
ukichezesha ligi ya mkoa (kwa maana yanyumbani na ugenini) ina maana bingwa wa
Wilaya ya Masasi atasafiri vipi akacheze Newala au Mkoani Lindi bingwa wa
Liwale atasafiri vipi akacheze na bingwa wa Kilwa, Pwani bingwa wa Mafia
atasafiri kwa gharama za nani akacheze Bagamoyo na wa Kibahaakacheze Utete?
Pamoja na nia njema ya TFF uhalisia hauruhusu.
Kama Mwenyekiti wa chamacha
mpira mkoa wa Kagera nalijua hili, hakuna haja ya TFF kuwa inatoa maelekezo
ambayohayatekelezeki, hasa ukizingatia kuwa TFF hakuna msaada wanaopeleka
kusaidia mikoa na wilaya ziandae mashindano yao. Vyama vya mikoa na wilaya
viachwe viendelee kutumiaubunifu wao kupata mabingwa wao kulingana na hali
halisi ya mazingira yao.
1.4 Kuanzisha mashindano mapya na
kufufua ya zamaniWataalam wa kandanda wanasema kuwa ili mchezaji awe katika
kiwango bora inabidi achezekwa mwaka kimashindano wastani wa mechi 40.
Ligi
yetu kuu,Vodacom premier league,inatoa fursa kwa mchezaji kucheza michezo 26
kwa mwaka iwapo anapangwa kilamechi.Hii haitoshi. Namna pekee ya kurekebisha
hali hii ni kuongeza idadi ya mashindano kwamwaka.Hili litafanyika kwa kufufua
kombe la Taifa (Taifa cup) na kuanzisha kombe lashirikisho (kama FA cup ya
Uingereza). Kombe la shirikisho litashirikisha timu zote nchinikuanzia ngazi ya
kata,tarafa,wilaya,mkoa hadi Taifa na bingwa wake atawakilisha nchi katikakombe
la shirikisho la Afrika CAF confederation cup (kama ilivyo Kenya kwa sasa).
.5. Mpira wa WanawakeHadi sasa hatuna
mfumo imara na unaoeleweka wa kuendeleza soka la kinamama. Mpira wawanawake
umeanzia Wilaya ya Kinondoni, ukakulia Wilaya ya Kinondoni na umegoteaWilaya ya
Kinondoni ambako kuna timu zenye majina kama Mburahati Queens na SayariQueens.
Mpira wa wanawake sharti usambae nchi nzima, na ili kufanikisha azma hii
lazimayaanzishwe mashindano ya kitaifa ya wanawake ikiwemo Ligi ya taifa ya
wanawake. Hiiitaendana na juhudi za kuongeza makocha, waamuzi na makamisaa
wanawake na kutafutaudhamini kwa timu ya Taifa ya wanawake TWIGA STARS.1.6
Maandalizi ya Vijana (Grassroot Programme)Mpango endelevu wa maendeleo ya soka
la vijana sharti uandaliwe, uratibiwe na kusimamiwakwa makini. Program madhubuti
ya maendeleo ya mpira wa vijana lazima ibuniwe ,iratibiwe
na kusimamiwa kwa usatadi
mkubwa.Mradi huu lazima ulenge ,kwa hatua,kufikia hatua yakuingiza timu zetu
fainali za kombe la Afrika la vijana chini ya umri wa miaka 17 na 20,fainaliza
olimpiki, fainali za Afrika wachezaji wa ndani CHAN,fainali za Afrika AFCON na
mwishofainali za kombe la dunia.Hii itakuwa ni pamoja na kujiwekea utaratibu wa
mzuri wakuhakikisha vijana wetu wanapata fursa ya kucheza mpira nje ya nchi ili
kujiongezeaumahiri.Na hii ni kwa wanawake na wanaume.Mpango huu ni lazima
ushirikishe Serikali Kuu (hasa Wizara zenye dhamana ya Michezo,Elimu na
Halmashauri), Taasisi zisizo za kiserikali,mashirika ya umma,sekta binafsi
naTFF,CAF na FIFA. Ushirikishwaji wa Serikali na Halmashauri katika program hii
ni muhimusana kwa kuwa ndio wasimamizi na wamiliki wa shule nyingi za msingi
ambako ndiko vijanawetu wanakoanzia kucheza mpira.
Mpango kazi huu lazima
uonyeshe:
1.Nini tunataka kufanikisha.
2.Utaratibu utakaotumika.
3.Nguvu kazi inayotakiwa na sifa
zake.
4.Mwongozo wa kufuatilia kupima ufanisi
wa programu.
5.Kupambanua gharama za mpango na
taratibu za uchangiaji wake.
Hatua muhimu katika kufanikisha program hii
zitakuwa ni:-Kufundisha walimu wa walimu (instructors), hawa ndio watakuwa
chachu ya kupatawalimu wa mpira mashuleni na mitaani.-Walimu wa walimu
(instructors) kufundisha walimu wa kutosha wa michezo mashuleni namitaani-Kwa
kushirikiana na wamiliki wa shule kuhakikisha viwanja vya kuchezea
vinakidhiviwango-Kutafuta na kusambaza vifaa vya michezo mashuleni hasa mipira
ya saizi muafaka kwamujibu wa viwango vya kimataifa.-Kupata shule angalau moja
kila mkoa itakayopokea watoto wenye vipaji maalum vyakucheza mpira, pale ambapo
wazazi hawataweza kuwalipia karo vijana hawa basi TFFihakikishe karo zao
zinapatikana,huo ndio uwekezaji katika mpira.-Kuandaa mashindano mbali mbali
yatakayoshirikisha shule hizi ili kupata timu za taifa zavijana wa umri mdogo
wa kike na wa kiume.-Kuhakikisha timu hizi za umri mdogo zinapata fursa ya kushiriki
mashindano mbali mbaliya kimataifa- Kupata vikosi vizuri vya timu za taifa za
vijana wa umri mdogo ambao watakua pamoja,hao ndio watajenga msingi imara wa
timu za Taifa za wakubwa kwa miaka ya baadae.Itakuwa ni muhimu sana program hii
iendane vizuri na ratiba nyingine za mashindano yakitaifa kama Umitashumta,
Umisseta, Airtel rising star, Copa Coca Cola n.k.
Kuanzisha mashindano ya kitaifa ya
kombaini za shule za sekondari na ya kombaini zavyuo vikuu. Wachezaji mahiri wa
timu ya taifa kama Leodeger Chilla Tenga (Rais waTFF) na Leopold Tasso Mkebezi
(meneja wa Taifa stars) waliibukia kwenyemashindano kama haya Mkebezi akiwa
beki wa kombaini ya sekondari zaBukoba,Ihungo,Kahororo na Nyakato.Aidha vituo
vya michezo (sports academies) ambavyo tayari vipo vitatengenezewa utaratibuwa
usajili na kuwekewa utaribu wa kuviendesha.Ili kuondoa ulalamishi wa vituo vya
mafunzo (Academies) kulalamikia malipo pindi mchezajiakisajiliwa timu kubwa,
vituo vyote vya vijana vitasajiliwa na vijana wao wote wataingizwakwenye
kumbukumbu za TFF (data base) kwa majina, saini na picha,hii itasaidia kuzuia
sakatakama la Mbwana Samata na klabu yake ya utotoni ya Mbagala maana
kumbukumbu za TFFzitakuwa ndio jibu la maswali yote.
1.7
Tiba
1.
Tutaimarisha usalama uwanjani.
Tutahimiza kila uwanja zinakochezwa mechi za ligi kuwe nagari la wagonjwa na
chumba cha dharura (emergency room).Katika kuimarisha usalama tutahakikisha
vifaa muhimu vya dharura kama vifaa vya hewa(oxygen) na vifaa vya kushtua moyo
(defibulator) vinakuwepo. Kwa sasa hapa Tanzaniauwanja pekee wenye vifaa hivi
ni Uwanja wa Azam Chamazi. Ni jambo la kusikitisha kuonahata uwanja mpya wa
Taifa hauna chumba cha tiba dharura (emergency room) na kibaya zaidimakato ya
uwanja hayaendi kuanzisha huduma hii muhimu wakati viongozi mbalimbali
wakitaifa wanahudhuria mechi uwanjani.2.
Mradi wa Goal Project wa FIFA unatoa
pesa za tiba na mradi huu uliweka lengo la kuwa nachumba cha kliniki pale
uwanja wa Karume. Tutakifufua chumba hiki, tutakiwekea vifaa nakuhakikisha
huduma ya kliniki kwa wanamichezo iliyokuwa ikitolewa na madaktari kilaJumapili
inarudishwa. Posho itatafutwa ili madaktari watoa huduma angalau wapate nauli
namaji ya kunywa.3.
Wakati wa kujadiliana mikataba na
wadhamini mbalimbali tutahakikisha kipengele chahuduma za afya kinaingizwa
katika mikataba. Udhamini utatafutwa kwa ajili ya vipimo vyawachezaji kabla ya
league (pre-league medical test) kama vile vipimo vya uvumilivu (Yo-Yotest) na
vipimo vya moyo (cardiac tests). Hii ni kwa ajili ya usalama wa wachezaji
nawaamuzi.4.
Hadi leo chama cha Madaktari
Tanzania, TASMA hakina ofisi. Hii ni aibu kwa chama chenyehadhi na umuhimu wa
kipekee kama hiki. Tutahakikisha TASMA inapata ofisi yake pamojana chumba
maalum cha kliniki.5.
Huduma ya afya lazima iwe sehemu
maalum ya mfumo wa idara ya ufundi. Ni muhimu timuya madaktari wa Timu ya Taifa
(National Medical team) ijulikane ni kina nani na wapewemikataba ya kazi. Hii
tutalipigania.6.
Majeraha ya michezo huwa yanahitaji
utaalam wake wa tiba. Tutaiomba Serikali itupeushirikiano ili kipatikane
kitengo maalum cha kutibu majeraha ya wanamichezo (sports
injuries wing) katika baadhi ya
hospitali zetu wakati tunajiandaa kuwa na kitengo cha tiba(Rehabilitation
Centre) katika kituo cha michezo kitakachojengwa.7.
Ili kuimarisha uwezo wa madaktari
wetu kutoa huduma za afya kwa wanamichezo,tutahakikisha madaktari wengi kadiri
iwezekanavyo wanapata kozi za msingi,kati na juu(preliminary,intermediate and
advanced). Nafasi hizi zitatolewa bila upendeleo wala kujuana.8.
Utoaji wa ushauri nasaha kwa
wachezaji utaongezeka hasa kuhusu masuala ya ukimwi namadhara ya madawa ya
kuongeza nguvu na ya kulevya.
.8
Waamuzi
Imepita miaka zaidi ya 15 toka
Tanzania itoe mwamuzi wa kimataifa wa kuchezesha fainali kubwa(mara ya mwisho
AFCON 1998), hii si sawa. Utaratibu uliopo sasa wa kuwapata na
kuwaendelezawaamuzi ama una mapungufu au haufai kabisa hivyo budi utafutwe
utaratibu ulio mzuri zaidi katikakupata waamuzi bora, tafiti zitafanywa ili
kubaini ni njia zipi za kisayansi za kuwapata waamuzi bora(Top referees).Semina
za mara kwa mara za CAF na FIFA ni nzuri lakini hazitoshi, TFF lazimaiwekeze
kwa kutoa mafunzo zaidi ya waamuzi kwa gharama zake.Aidha mradi wa maendeleo ya
mpira kwa vijana (grassroot) utahusisha pia mafunzo ya uamuzi wampira kwa
vijana kama kinavyofanya kituo cha Jenerali Twalipo.Utaratibu wa kutoa adhabu
kwa waamuzi wanaosemekana wameboronga uwanjani nao unahitajimarekebisho ya
haraka sana. Uamuzi wa mpira ni taaluma kama zilivyo taaluma
nyingine,mwamuziakikosea ni vyema akakosolewa na mwamuzi mwenzie ambaye ni
mwandamizi,na kama nikuadhibiwa aadhibiwe na jopo la waamuzi wenzie waandamizi
lakini wastaafu na sio mtu mwingineambaye hajawahi kupuliza filimbi.1.9
Makocha
Kumekuweko na utamaduni usiofaa
katika soka la Tanzania miaka ya karibuni wa kuona kuwamakocha wa kigeni ndio
bora zaidi na wanastahili mikataba,mishahara minono na marupurupuilhali makocha
wazawa wanageuzwa ‘deiwaka’, jambo hili ni baya sana,ajira ziheshimiwe
kwamsingi wa taaluma na sio kwa msingi wa nchi atokayo mtu.Makocha wetu
wazalendo wana uwezo mkubwa kama wakipewa nyenzo kama wanazopatiwawageni, kama
malipo mazuri, mikataba ya muda mrefu, vitendea kazi na kuheshimiwa programzao
bila kuingiliwa na viongozi.Iwapo nitachaguliwa ninaahidi:- Kuwaendeleza
makocha kimafunzo ndani na nje ya nchi kwa wale wenye uwezo nautashi wa kufanya
hivyo.- Kushawishi taasisi za elimu nchini kama vyuo vikuu kufundisha taaluma
ya ukocha- Kuhakikisha walimu wa mpira wa timu zetu za Taifa wanakuwa na
mikataba stahiki, hiini pamoja na benchi zima la ufundi.
- Kuwajengea uwezo makocha wetu
wazalendo ili nao wapate fursa ya kufundisha mpiranje ya nchi.- Kuanzisha tuzo
za kila mwaka za makocha wazalendo ambao wamefanya vizuri katikaufundishaji wa
soka la vijana la wanawake na wanaume.- Kuhakikisha utaratibu wa leseni za CAF
unazingatia vigezo vya kitaaluma, uzoefu naushiriki wa kocha mhusika katika
ufundishaji. Makocha ambao wanafundisha (activecoaches) watapewa kipaumbele
katika kupata kozi za kupanda madaraja kuliko walewanaofungia vyeti
makabatini.Leseni za CAF ni muhimu katika kumfanya mwalimu wampira atambulike
kimataifa.- Kuhakikisha kanuni za ligi zinasimamiwa vyema ikiwemo kanuni
itakayomlazimishakila mwalimu wa ligi kuu na daraja la kwanza awe mwanachama wa
TAFCA (chamacha makocha nchini), walimu wa kigeni watapewa uanachama wa
muda.1.10
Timu za Taifa
Timu zetu za Taifa, ziwe za wakubwa
au za vijana ndio kioo cha mpira wa Tanzania. Jitihadazote lazima zifanyike
kuhakikisha tunakuwa na timu nzuri za Taifa kuanzia za
wakubwa(wanawake/wanaume) hadi za vijana. Pamoja na jitihada zitakazofanyika
kuboresha idara yaufundi kama ilivyoanishwa hapo juu lakini pia yafuatayo ni
mambo ya ziada yatakayofanyika.
(a)
Kuandaa fainali za Afrika za umri
chini ya miaka 17 (U-17) mwaka 2019
Hadi sasa hakuna nchi ambayo
imekwisha pata uenyeji wa mashindano haya. Uenyeji huuunatolewa na Shirikisho
la vyama vya mpira Afrika CAF.Hii ni changamoto kwetuWatanzania kuomba uenyeji
huu.Tukipewa fursa hii itatusaidia sana kutusukuma tuanzekuandaa programu ya
nguvu ya miaka mitano ya kupata timu yetu itakayocheza katikafainali hizi kama
wenyeji. Aidha kama nchi tutalazimika kuboresha miundo mbinu yetuhususani
viwanja vyetu vya mpira, jambo ambalo litatusaidia siku za usoni.
Ninaaminiuwezo wa kuandaa mashindano haya kama nchi tunao. Nikichaguliwa
nitalisimamia hili.
(b)
Nidhamu
TFF itaandaa Kanuni za Nidhamu (code
of ethics) kwa wachezaji, walimu na viongozi waTimu za Taifa mara wawapo ndani
na nje ya uwanja. Hii itasaidia kujenga nidhamu yatimu. Kanuni hizi zitaendana
sambamba na kanuni za maadili za TFF.
(c)
Walimu
Ni vyema siku za usoni timu zetu zote
za Taifa zikafundishwa na makocha wazawa.Utaratibu utafanyika kuhakikisha
makocha wasaidizi ambao ni wazawa wanaendelezwakufikia kiwango hicho, hii
itakuwa ni pamoja na kuwapatia fursa za mafunzo ndani na njeya nchi.
d)
Zanzibar
TFF kwa kushirikiana na Chama cha
Mpira Zanzibar ZFA tutahakikisha kunakuwa namahusiano ya karibu ya walimu wa
timu za Taifa Zanzibar na Bara ili kuhakikisha timu bora ya Taifa inaundwa na
vijana wa pande mbili za Muungano. Aidha jitahada za Zanzibar kuwa mwanachama
kamili wa CAF na FIFA zitaendelea kuungwa mkono.
2.
Utawala
Inabidi tuendeleze utamaduni wa
kuendesha shughuli za TFF kitaasisi (to have a corporateculture).Nguzo muhimu
za uendeshaji shirikisho kitaaluma ni pamoja na kujenga nidhamu
yawafanyakazi,heshima kwa uongozi,utunzaji wa kumbukumbu,ukarimu kwa
wageni,umakinikatika manunuzi na utunzaji wa fedha pamoja na kufanya kazi kwa
malengo na kuhakikishamalengo hayo yamefikiwa.
Maeneo yafuatayo yataboreshwa ili
kuongeza ufanisi:
2.1 Ofisi za Mikoa na Vyama ShirikiKwa
kuzingatia vyama vya Mikoa kuwa ndio muendelezo mkuu wa shughuli za TFF
Mikoani,ni muhimu ofisi za mikoa zikawa kielelezo cha ufanisi wa utendaji wa
TFF. Ofisi za Mikoazitaboreshwa hasa kwa kupewa vitendea kazi hususani vifaa
vya mawasiliano.Vyama shiriki hadi sasa havina ofisi zenye hadhi ya vyama hivi,
tutahakikisha tunaondoa aibuhii. Aidha kutokana na mapato ya TFF sehemu ya
mapato haya itatengwa kwa ajili ya ruzukuya kupeleka kwenye vyama vya Mikoa na
vyama shiriki ili isaidie kupunguza makali yakuendesha vyama vyetu.2.2
Ofisi ya RaisKutakuwa na ofisi ya
Rais wa TFF. Ofisi ya Rais wa TFF (office of the President) lazimaiimarishwe na
iwe sehemu itakayoweza kukabiliana na changamoto za maendeleo ya mpirawa miguu.
Rais wa TFF ndiye msimamizi mkuu wa shughuli za mpira wa nchi hii,lazimaawe na
mahali stahili pa kufanyia kazi kulingana na hadhi yake.Hii itakuwa ni pamoja
nakuwa na wasaidizi wenye uweledi wa kutosha katika shughuli za kila siku za
kuongozashirikisho.Ofisi za TFF makao makuu uwanja wa Karume zitakarabatiwa na
kuongeza nafasi yakufanyia kazi.2.3 MaslahiMaslahi ya wafanyakazi wa TFF
yataboreshwa ili kuwaongezea motisha. Hii itakuwa ni pamoja na kuwapa fursa ya
kuhudhuria mafunzo mbalimbali.
2.4 Vilabu vya MpiraVilabu
vitasaidiwa kupewa mwongozo wa kujiendesha kwa ufanisi zaidi. Aidha utaratibu
wamgawanyo wa mapato ya milangoni utatazamwa upya kwa lengo la kuhakikisha
vilabuvinapata mgao mkubwa kuliko iliyo sasa. Hii ni kwa kuzingatia gharama
kubwa wanazoingiavilabu katika kuandaa timu ikiwemo malazi, usafiri, vifaa,
posho, dawa, mishahara n.k.2.5 Wachezaji wastaafuHii ni hazina ya
Taifa,kustaafu kwao kucheza mpira sio mwisho wao wa kuchangia maendeleoya mpira
wa nchi yetu.Jitihada zitafanyika kuanzisha mfuko maalum (Trust Fund)
ambaoutachangiwa na wachezaji wenyewe wanapokuwa bado dimbani pamoja na TFF,
hii ni kwa ajiliya kuwasaidia hapo baadae wanapokuwa na matatizo hasa ya
ugonjwa. Aidha chama chawachezaji wastaafu (SPUTANZA) kitapewa ofisi na
kitaimarishwa ili kiwe kiungo muhimukati ya wachezaji na TFF.Wachezaji
watahimizwa watumie chama hiki kutatua matatizo yao nachama kitapewa fursa
kikanuni ya kuwa mtetezi mkuu na msimamizi wa maslahi ya wachezaji.
2.6 MikatabaUtaratibu wa TFF kuingia
mikataba na wadhamini mbalimbali utarekebishwa ili kuongezauwazi. Ipo mikataba
ambayo imesainiwa na TFF ambayo imesababisha vyama vya mikoa nawilaya, pamoja
na uhaba wao wa pesa, wahangaike kutafuta fedha za zaida kuandaa timu zaokwa
ajili ya mashindano yanayobeba jina la mdhamini kwa kuwa fedha anayotoa
mdhaminihaikidhi uendeshaji wa mashindano yenyewe.Aidha vipengele tata
vinavyokandamiza maslahi ya vilabu katika baadhi ya mikatabainayosainiwa kati
ya TFF na wadhamini vitarekebishwa kama sio kuondolewa kabisa kwamaslahi ya
ustawi wa mpira wetu. Haki za vilabu katika matangazo ya biashara yahusuyompira
zitalindwa kwa nguvu zote.
1.
TFF
inatengeneza utaratibu mzuri wa kuuza bidhaa zake ndani na nje ya nchi kwa
kupitiauuzaji wa kawaida na wa mtandao.Mikataba itaandaliwa ili kudhibiti
uuzwaji holela wa bidhaa za TFF.2.
Vyumba vya
Maduka vinajengwa kuzunguka uwanja wa Karume na kukodishwa.3.
Jengo la
kitega cha uchumi litajengwa kwenye ardhi ya Uwanja wa Karume.Pia jukwaa lawatazamaji
litajengwa uwanja wa Karume ili mechi ambazo sio kubwa ziweze
kufanyika pale, hii itaviongezea vilabu mapato.4.
Juhudi za
kuboresha ukusanyaji, usimamizi na mgawanyo wa haki wa mapato ya
milangoniyatokanayo na ligi yetu utaboreshwa ikiwa ni pamoja na kubuni vyanzo
vipya kupitia njiambali mbali zikiwemo za udhamini mbadala kwa vilabu.Aidha
jitihada ambazo tayarizimekwisha anza za kuunda bodi ya kuendesha ligi na
uanzishwaji wa utaratibu huru wakuendesha ligi zitaendelezwa ili kuongeza
ufanisi,kuinua mapato ya vilabu na kuongezamsisimko wa ligi.Ninaunga mkono
juhudi hizi.
5.
Viwanja
vingi vya mpira nchini vinamilikiwa aidha na Halmashauri,Serikali kuuau vyama
vya siasa.Viwanja hivi vingi viko katika hali mbaya kuanzia nyasi ,haliya
uzio,vyumba vya kubadilishia nguo,mageti,vifaa vya kuzimia moto n.k.nivyema TFF
na vyama vya mikoa kwa kupitia utaratibu wa PPP (Public PrivateSector
Partnership) vikaingia ubia na wamiliki wa viwanja hivi ili TFF nawashirika
wake wachukue jukumu la kuviboresha,kuvisimamia na kuviendesha ilikuhakikisha
vinakuwa katika viwango stahili kwa mujibu wa kanuni za FIFA naCAF.Hii
itaongeza usalama wa wachezaji na watazamaji na kuinua mapatoyatokanayo na viwanja hivi
Ushiriki
wa wadauKwa sasa taswira ya mpira wa miguu inawafungia nje wadau wengi ambao
kama wangepewa fursaya kushiriki nao wangetaka wachangie maendeleo ya mpira wa
miguu.Juhudi kubwa inabidi zitumikekurudisha imani hii ili kuleta hisia za
umoja wa kitaifa katika kuendesha mpira wetu (sense of belongingness)
.Ni muhimu taasisi muhimu za kitaifa zishirikishwe katika sekta hii ya mpira
wamiguu ,hii ni pamoja na taasisi kama Tacaids,Mashirika ya utalii kama TANAPA
na TTB,Umoja wawafanyabiashara kama TPSF,CTI na TCCIA ,Kituo cha uwekezaji TIC
n.k.Ushirikiano huu utasaidiakujenga jina la Tanzania pale tunapoandaa michuano
ya kimataifa na pia kuhamasisha vijana wetuwaepuke maisha hatarishi kama vile
kujihusisha na ngono isiyokuwa salama,madawa ya kulewa(kutumia na
kusafirisha),ulevi wa kupindukia n.k.
HITIMISHO
Ndugu
zangu,nihitimishe kwa kusisitiza kuwa maendeleo ya mpira Tanzania kwa
hapayalipofikia yanahitaji ubunifu,ujasiri na msukumo mpya ili tuweze
kuunyanyua mpira wetu nakuupa mwelekeo mpya,mwelekeo wa matumaini ,mwelekeo wa
kulipeleka soka letu katikakushinda vikombe vikubwa barani mwetu Afrika na
Duniani.Shime wapiga kura nipeni fursa hii ya kuwa Rais wa TFF ili kwa pamoja
tukishirikiana nawadau wote muhimu katika sekta yetu tuweze kulisikuma gurudumu
hili ili hatimae soka iwezekuiletea nchi yetu sifa na kuwapa raha mamilioni ya
watanzania wapenda mpira.Pamoja tutawezaChagua MALINZIChagua MABADILIKOMungu
ibariki AfrikaMungu ibariki TanzaniaJamal MalinziMgombea nafasi ya UraisTFF2013
Mpira ni
afya, mpira ni burudani, mpira ni ajira kwa vijana!
MAELEZO
BINAFSI YA JAMAL EMIL MALINZI MGOMBEA URAIS TFFTarehe ya kuzaliwa
: 08 Agosti,
1960
Elimu
:
1974-1977 : Sekondari O-LevelMwanza Secondary School1978-1981 : A-LevelIlboru
High School1980-1981 : JKT – RuvuOperesheni TIJA1981-1985 : Chuo Kikuu Dar Es
SalaamDigrii ya Uhandisi (Upper 2
nd
Class)1986-1993
: Ajira -Coopers
and Lybrand Tanzania Industrial Researchand Development
Organization1993-Hadi Leo : MjasiriamaliMkurugenzi – Cargostars Limited
Michezo
: Nimekuwa
promota wa mchezo wa ngumi za kulipwakuanzia
kipindi cha 1995-2001. Baadhi ya mabondiawangu walifikia kiwango cha
kimataifa hadi kusainimkataba na Promota maarufu duniani Don King.: Nimekuwa Seneta
wa Yanga na baadae nikawaMkurugenzi na mwisho nikawa Katibu Mkuu wa Klabuya
Yanga kati ya mwaka 1999 na 2005.: Nimekuwa Mkurugenzi na Msimamizi Mkuu wa
Timu yaMkoa wa Dar Es Salaam ya Mzizima United. Timu hiindiyo ya mwisho
kushinda Kombe la Taifa mwaka 2007ikiwa timu moja ya Mkoa wa Dar Es Salaam.:
Nimekuwa mjumbe wa Baraza la michezo la mkoa waDar es salaam 2009-2011:
Nimekuwa Mwenyekiti wa kamati ya mashindano mkoawa Pwani 2009-2011: Hadi sasa
mimi ni mwenyekiti wa Chama cha mpira wamiguu mkoa wa Kagera: Kikampuni, Kampuni
yetu ya Cargostars Limited inauzoefu wa muda mrefu wa kudhamini
michezombalimbali. Kwa kipindi cha miaka saba CargostarsLimited iliidhamini
mbio za marathon za wabunge.Aidha Cargostars Limited ina rekodi ya
kudhaminimichezo mingine kadhaa ikiwemo mpira wa miguu, ngumi,
Tennis na Golf.
No comments:
Post a Comment