Arsenal imemuongeza katika orodha ya kitabu chao cha usajili wa vijana mlinda mlango wa Bristol Rovers Matt Macey.
Mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 18 atakuwa akielekea Emirates Stadium baada ya kumvutia meneja wa Arsenal Arsene
Wenger na jopo lake la ufundi wakati wa kipindi cha maandalizi ya msimu mwezi uliopita.
Macey amekuwa katika mawindo mengine kutoka katika vilabu kama Everton na vilabu vya ligi ndogo ya Championship lakini lakini inadhaniwa kuwa ameelekeza moyo wake London ya kaskazini.
No comments:
Post a Comment