Kinyang'anyoro cha Champions League kinarejea uwanjani usiku huu wa Jumanne kesho Jumatano. Arsenal ya London na Barcelona ni timu mbili ambazo zinawania
kupata ushindi wa tatu katika michezo mitatu ya makundi yao.
Viongozi hao wa Premier League Arsenal na Borussia Dortmund makamu
bingwa wa Champions League walikutana katika msimu wa mwaka 2011-2012
wakati Robin van Persie alipofanikiwa kufunga katika mchezo wa nyumbani .
Mchezo wa pili ulikuwa sare ya bao 1-1 mjini Dortmund.
Schalke 04 pia itakuwa uwanjani usiku huu ikioneshana kazi na
Chelsea, Chelsea inahitaji kwa udi na uvumba ushindi mjini
Gelsenkirchen kupata kujiamini zaidi baada ya ushindi wao wa mabao 4-0
dhidi ya Steaua Bucharest katika kundi E.
Michezo mingine ni kati ya
Steaua Bucharest ikiikaribisha Basel ya Uswisi, Marseille ya Ufaransa
inakuwa mwenyeji wa SSC Napoli ya Italia, wakati katika kundi G , Porto
ya Ureno imewaalika Zenit St Petersburg ya Urusi.
Austria Vienna ina
kazi dhidi ya Atletico Madrid , na Celtic itakuwa kibaruani na Ajax Amsterdam
ya Uholanzi katika kundi H, ambapo pia AC Milan inaikaribisha nyumbani
Barcelona.
Michezo hiyo inaendelea hapo kesho Jumatano ambapo mabingwa Bayern Munich
inawakaribisha Pilsen ya Denmark na Leverkusen wako nyumbani
kuikaribisha Schachtar Donetzk ya Ukraine.
No comments:
Post a Comment