KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, October 4, 2013

JUAN MATA AITWA KIKOSINI HISPANIA LAKINI DIEGO COSTA AKOSA NAFASI MAJERUHI TORRES, ALONZO, ALABA NA CAZORLA WAACHWA.

Bosi wa kikosi cha timu ya taifa ya Hispania Vicente del Bosque amemuita tena Juan Mata katika kikosi cha timu ya taifa ya cha nchi hiyo kujiwinda na michezo dhidi ya Belarus and Georgia.

Kiungo wa Chelsea alikuwa vizuri katika kikosi cha timu yake ya Chelsea chini ya Jose Mourinho lakini kumbukumbu ikionyesha kuwa kiungo huyo alikosekana katika michezo mitatu ya hivi karibu ya Hispania kutokana na kukosa kiwango lakini sasa atakuwepo katika kikosi cha wachezaji 23 kwa ajili ya michezo miwili ya kufuzu kombe  la dunia Oktoba 11 na 15.

Nyotab wa Atletico Madrid Mario Suarez na Koke wote wamerejeshwa kikosini kama ilivyo kwa kiungo wa Real Madrid Isco, licha ya kwamba mshambuliaji wa Tottenham Roberto Soldado akikosa nafasi nafasi katika kikosi hicho cha Hispania.

Ntota wa Manchester City Alvaro Negredo na David Villa ni washambuliaji wa kati walio ingizwa kikosini.
.
Wakati huo huo Alberto Moreno wa Sevilla ameitwa kwa mara ya kwanza ingawaje Diego Costa mzaliwa wa Brazil aliye pewa uraia wa Hispania akikosa nafasi tofauti na ilivyotegemewa hapo kabla ambapo shirikisho la soka la Hispania  (RFEF) likisubiri kupokea uthibtisho ambao utamuhalalisha kuwakilisha kikosi cha la Roja.

Majeruhi Xabi Alonso, Jordi Alba, Santi Cazorla na Fernando Torres wote hawatakuwepo kikosini lakini mlinda mlango Iker Casillas akiendelea kupata nafasi kikosini.
Spain kwasasa wanaongoza kundi I kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa dhidi ya France na bado wana mchezo mmoja pungufu tofauti na kikosi cha kocha Didier Deschamps wa Ufaransa.

Squad in full:
Goalkeepers: Iker Casillas (Real Madrid), Jose Reina (Napoli), Victor Valdes (Barcelona)
Defenders: Alvaro Arbeloa (Real Madrid), Juanfran (Atletico Madrid), Gerard Pique (Barcelona), Raul Albiol (Napoli), Sergio Ramos (Real Madrid), Ignacio Monreal (Arsenal), Alberto Moreno (Sevilla).
Midfielders: Sergio Busquets (Barcelona), Mario Suarez (Atletico Madrid), Xavi Hernandez (Barcelona), Andres Iniesta (Barcelona), Koke (Atletico Madrid), Isco (Real Madrid), Pedro Rodriguez (Barcelona), Jesus Navas (Manchester City), Cesc Fabregas (Barcelona), Juan Mata (Chelsea), David Silva (Manchester City).
Forwards: Alvaro Negredo (Manchester City, David Villa (Atletico Madrid).

No comments:

Post a Comment