Mshambuliaji timu ya taifa ya Ghana Andre Ayew
hataweza kucheza kwa takriban kipindi cha majuma manane baada ya kutegua
goti.
Kijana huyo wa umri wa miaka 23 aliumia goti
lake wakati wa pambano la mkondo wa pili dhidi ya Misri katika
kinyang'anyiro cha nafasi za fainali ya kombe la dunia siku ya jumaanne.
Klabu yake ya Marseille ya Ufaransa ilisema
katika wavuti wake kwamba Ayew alipimwa na madaktari na kupatikana
ametegua goti lake na atafanyiwa operesheni siku ya Jumaatatu.
Hili ni pigo kubwa kwa Ayew, ambae amekua
akitamba katika michezo ya hivi karibuni na akifunga mabao manne katika
michuano tisa aliyokwishacheza.
Ghana ilipoteza mechi ya mjini Cairo 2-1 lakini
ikafaulu kucheza katika michuano ya fainali ya kombe la dunia nchini
Brazil hapo mwakani kw akuibuka na ushindi wa jumla ya mabao7-3.
No comments:
Post a Comment