KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, December 6, 2013

CECAFA CHALLENGE CUP: VUTA NIKUVUTE NI HAPO KESHO ROBO FAINALI SOMA RATIBA.

Ratiba ya Robo fainali ya Chalenji
CECAFA 2013 QUARTER-FINALS (In Mombasa):
Saturday December 7, 2013
Uganda Vs Tanzania – 2pm
Kenya Vs Rwanda – 4pm
Sunday December 8, 2013
Zambia Vs Burundi – 2pm
 Ethiopia Vs Sudan – 4pm
Hakuna shaka kuwa viwanja wa vya Afraha Nakuru na Kenyata Machakakos vimeweka historia ya kuingiz watu wengu zaidi katika michuano ya mikongwe kuliko yote barani Afrika ya CECAFA 2013 msimu huu wa mwaka 2013.
Tofauti na ilivyokuwa jijini Kampala msimu uliopita ambapo viwanja vilikuwa havina mashabiki ukiachilia mbali uwanja wa Nelson Mandela Stadium kule Namboole.
Waratibu wa michuano safari hii wamejitahidi kuongeza hamasa na kuvutia watazamaji wengi kwa kuisambaza michuano hiyo katika miji tofauti katika hatua ya makundi.
Akinukuliwa katibu mkuu wa CECAFA Nikolaus musonye amesema 
"Soka nchini Kenya si kama ilivyo katika miji ya Dar es Salaam au Kampala ambapo mashabiki wanaingia wakati wote. hapa mashabiki wanafurahia zaidi vilabu vyao kuliko timu za taifa".

Mgavana nchini Kenya wamechukulia mashindano kwa hamasa kubwa na kuipeleka katika miji yao ya Kisumu, Nakuru, Machakos na Mombasa na hivyo kuongeza watazamaji kuwa tayari.

Mashabiki hawakuvunjwa moyo katika miji ya Nakuru na Machakos ambako michezo ilikuwa michache kuliko Nairobi ambako kuna viwanja viwili vya Stadia of Nyayo  City Stadium.

No comments:

Post a Comment