GOALS GALORE
Manchester City imekamilisha idadi ya magoli 35 ndani ya michezo nane ya Premier League katika uwanja wa nyumbani Etihad ndani ya msimu huu.
Hull City ndiyo timu pekee kuondoka Etihad ikifungwa idadi ndogo ya mabao yaani chini ya mabao mawili.
Angalia vichapo cha Etihad msimu huu
4-0 vs Newcastle
2-0 vs Hull
4-1 vs Manchester United
3-1 vs Everton
7-0 vs Norwich
6-0 vs Tottenham
3-0 vs Swansea
6-3 vs Arsenal
Manchester City imejiweka katika nafasi nzuri ya kuwania taji msimu huu baada ya kuwanyoa bila maji vinara wa ligi ya England Arsenal kwa mabao 6-3 ndani ya uwanja wake wa nyumbani Etihad.
Safu ya ushambuliaji yenye makali ya kusisimua na uchu wa hali ya juu ya Sergio Aguero na Alvaro Negredo ndiyo iliyokuwa mwiba huku Fernandinho akizamisha wavuni mara mbili na David Silva na Yaya Toure
wakiingia katika orodha ya wafungaji katika mchezo huo.
Kwa upande wa Arsenal Theo
Walcott kwake ulikuwa ni mchezo wa kwanza kuonekana uwanjani tangu mwezi Septemba akitupia nyavuni bao mbili huku Per Mertesacker pia alipata nafasi ya kufunga bao la kichwa katika dakika za lala salama na kukamilisha mabao matatu ya kufutia jasho kwa Arsenal.
Jumping for joy: Manchester City narrowed the gap to Arsenal with thrilling victory over the league leaders
MATCH FACTS
Man City: Pantilimon
6, Zabaleta 8, Demichelis 7, Kompany 8, Clichy 6, Nasri 7 (Javi Garcia
90), Fernandinho 9, Toure7 , Silva 8 (Milner 71, 7), Aguero 7 (Jesus
Navas 50, 7), Negredo 7.
Subs not used: Hart, Lescott, Dzeko, Kolarov.
Booked: Kompany, SIlva.
Goals: Aguero 14, Negredo 39, Fernandinho 50, 88, Silva 66, Yaya Toure 90.
Arsenal: Szczesny 6, Sagna 5,
Mertesacker 7, Koscielny 6 (Vermaelen 42, 6), Monreal 6, Ramsey 6,
Flamini 6 (Gnabry 72, 6), Walcott 7, Ozil 6, Wilshere 7, Giroud 6
(Bendtner 76, 6).
Subs not used: Rosicky, Arteta, Cazorla, Fabianski.
Booked: Szczesny.
Goals: Walcott 31, 63, Mertesacker 90.
City sasa imefanikiwa kufunga jumla ya mabao 35 katika jumla ya michezo yake nane iliyocheza uwanjaw nyumbani msimu huu na ilistahili alama tatu ambazo sasa zimeifanya timu hiyo kufikisha alama 32 ikiwa ni alama 3 nyuma ya vinara hao wa ligi Gunners.
Kitu ambacho ni hasara kwa kocha Manuel Pellegrini ni kumpoteza mshambuliaji wake Aguero mapema katika kipindi cha pili kufuatia kupata maumivu ya msuli.
City imeendeleza rekodi yake nzuri ya asilimia 100 ya matokeo mazuri ya uwanja wa nyumbani.

No comments:
Post a Comment