KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, December 14, 2013

Mfanyakazi mwingine wa uwanja wa kombe la dunia Brazil adondoka na kufariki dunia

Mfanyakazi wa moja ya viwanja vya kombe la dunia aliyedondoka kutoka katika paa la uwanja wa Amazon ambao Engalnd itafunga michezo yake ya kombe la dunia amefariki dunia.
Mtu huyo inaarifiwa kuwa amefariki dunia hospitali Manaus kufuatia kudondoaka kutoka umbali wa mita 35 metres au futi 115 kufuatia kuvunjika kwa kebo.
Uwanja huo uko nyuma ya ratiba yake ya ujenzi na ujenzi wake umekuwa ukiendelea usiku na mchana ili kukamilisha kwa wakati kabla ya muda wa mwisho uliopangwa na Fifa.

Hizi ni taarifa mfululizo za matukio ya vifo wakati wa ujenzi wa viwanja vya fainali za kombe la dunia zitakazo fanyika nchini Brazil mwezi juni.
Watu wawili walifariki dunia kwa ajali iliyotokea mwezi Novemba 27 kwa ajali ya krane kudondoka na kuharibu sehemu ya uwanja wa Sao Paulo wa Arena Corinthians ambao utatumika kwa mchezo wa hafla ya ufunguzi wa fainali hizo.

Mfanyakazi huyo aliyefariki dunia anaitwa Marcleudo de Melo Ferreira, aliyekuwa na umri wa miaka 22.

Taifa hilo pia limekuwa likikumbwa na maandamano ya raia wa nchi hiyo ambao wamekuwa wakilalamikia matumizi makubwa na matumizi ya rasilimali za nchi. 

Wiki iliyopita katibu mkuu wa Fifa Jerome Valcke amewataka wananchi wa Brazil kuiunga mkono nchi yao.

No comments:

Post a Comment